Friday, June 17, 2016

Wabunge UKAWA Wasusa Futari ya Waziri Mkuu

 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisikiliza neon la shukrni kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia
Ackson mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa jana walisusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ikiwa ni mwendelezo wa hatua za kususia shughuli zote zinazoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Riziki Ng’wale, alisema wamechukua hatua hiyo kutokana na Dk Tulia kuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo.
“Dk Tulia ndiye mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kufuturisha na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki shughuli yoyote inayoongozwa naye,” alisema muda mfupi baada ya kutoka katika kikao cha wabunge wa kambi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema wamekubaliana wabunge wote wa kambi ya upinzani waliofunga watakwenda kufuturu majumbani kwao.
“Tumekubaliana hatutakwenda kufuturu bungeni na kila mbunge atakwenda kufuturu nyumbani kwake,” alisema.
Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha wapinzani kilichoketi chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.
Futari hiyo ilitangazwa na Dk Tulia tangu juzi na kusisitizwa jana baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa mchana kuwa ingefanyika kwenye viwanja vya Bunge ambako wabunge wote walialikwa.
Kwa siku zaidi ya 10 sasa, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk Tulia kwa sababu hawana  imani naye.
Hali hiyo imefanya bajeti kuu kwa ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuchangiwa na wabunge wa CCM tu baada ya Dk Tulia kuongoza vikao kila siku, akiingia asubuhi na jioni


   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwaongoza wabunge kupata futari iliyoandaliwa na Wazri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt Tulia Ackson akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa mara
baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu akitoa neon la shukrani kwa Wazri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa mara baada ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Mhe. Andrew Chenge akitoa neon la shukrani kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwashukuru wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mara baada ya kujumuika naye katika futari aliyowaandalia leo na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

No comments: