Thursday, June 16, 2016

WATOTO WAENDELEA KULILIA SHERIA KANDAMIZI,IPO PIA SHERIA YA NDOA,TIZAMA MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRICA KUTOKA LHRC LEO


 Na Vicent Macha-Dar es salaam

Ikiwa Tanzania na Africa tukiadhimisha siku ya mtoto wa Africa siku ya kukumbuka watoto Zaidi ya 300 waliouwawa nchini Africa kusini wakiwa katika maandamano,Seriali ya Tanzania kupia Bunge lake wametakiwa kufanya marekebiho sheria zote nchini ambazo zinamkandamiza mtoto pamoja na kuhakikisha kuwa sheria zilizopo kuhusu mtoto zinatekelezwa kwa umakini na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaofanyia watoto vitendo vya ukatili.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na watoto kutoka shule mbalimbali walipokuwa wanatoa maoni yao katika maadhimisho yaliyoandaliwa na kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini LHRC kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo ambapo wamesema kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria nyingi za kumlinda mtoto nchini lakini bado kuna sheria kandamizi kwa motto ambazo zinahitaji mabadiliko ya haraka kwa kuwa zinazidi kuwaumiza watoto nchini.

GLORIA SAMBO ni mwanafunzi aliyesoma hotuba kwa niaba ya wenzake ameeleza kuwa vitendo vya ukandamizaji nchini bado vinashamiri ambapo ametolea mfano swala la wazazi na walezi kuwakutuma vileo watoto wao pamoja na kwenda nao katika kumbi za starehe mambo ambayo yanahitaji kusimamiwa na serikali na sheria kuchukua mkondo wake mara moja.
Mwanafunzi GLORIA SAMBO akisoma Hotuba ya watoto hao kwa niaba ya wenzake katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto Frica yaliyoadhimishwa na Kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini LHRC Jijini Dar es salaam
Ametaja pia swala lingine ni maaswala mazima ya ajira za utotoni,kutoroshwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutumikishwa,biashara za ngono kwa watoto,watoto kushirikishwa katika biashara za madawa ya kulevya,na kuwauwa kwa Imani za kishirikina pamoja na adhabu kali kutoka kwa wazazi na walezi mambo ambayo yote yametajwa kuwa serikali inatakiwa kusimamia sheria ili kuwalinda watoto na maswala hayo.

Moja kati ya sheria ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa maswala ya haki za watoto ni pamoja na sheria ya motto ya mwaka 2009 kwenye maswala ya ndoa ambapo inakinzaa na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi na miaka 14 kwa ridhaa ya mahakama,hali ambayo inafanya Tanzania kuwa kati nchi zenye kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni kwa nchi za Africa.

Akizungumza na watoto hao Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELEN KIJO BISIMBA leo katika maadhimisho hayo ya mtoto wa Africa  yaliyoadhimishwa na LHRC Jijini Dar es salaam.
Watoto hao wameitaka serikali kuiagalia upya sheria hiyo kwani ni sheria kandamizi moja wapo katika nchi na imekuwa ikigharimu maisha ya watoto wengi kupoteza haki zao za msingi.


Aidha katika hatua nyingine watoto hao wametoa wito kwa watanzania kwa Ujumla kuheshimu haki za mtoto,pamoja na makundi muhimu yenye ushawishi katika jamii wakiwemo viongozi wa dini kuhubiri haki za watoto na kuwatahadharisha wanajamii wanaowaongoza kuwa na hofu ya mungu ili kuepuka kutenda dhambi ikiwemo uvunjaji wa haki za mtoto.
Akizungumza na watoto hao Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Mama HELEN KIJO BISIMBA amesema kuwa katika maswala ya watoto kila mtanzania anastahili kuhusika kikamilifu katika kulinda na kuheshimu haki za mtoto na sio jukumu la mtu Fulani au serikali pekee bali ni jukumu la watu wote.


Siku ya mtoto wa Africa huazimishwa kote barani Africa kwa lengo la kutambua thamani utu umuhimu wa mtoto duniani ikiwa ni kumbukumbu ya watoto 300 waliouwawa nchini Africa kusini ambapo nchni Tanzania kauli mbiu ni kupambana na mila potofu zinazomkandamiza mtoto na tabia zote mbaya dhidi ya mtoto.
PICHA NYINGINE ZA SHUGHULI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WATOTO HAO ZIKIWEMO MAIGIZO NA MICHEZO MBALIMBALI KAMA ISHARA YA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRICA.






No comments: