Saturday, July 16, 2016

ASKOFU DK. CHARLES GADI KUONGOZA MKUTANO MKUBWA WA KUOMBEA TAIFA VIWANJA VYA BIAFRA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Good News for All Ministtry (Great Vition 2000), Askofu Dk.Charles Gadi (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkubwa wa kuombea Taifa kila Jumanne kwa siku 1001 utakaofanyika kuanzia Julai 19, 2016 viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mchungaji James Manyama, Palemo Massawe na Mchungaji Leonard Kajuna.
 Mchungaji Palemo Massawe (kulia), akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu mkutano huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askofu Dk. Charles Gadi (wa pili kushoto), na wachungaji wenzake wakiomba baada ya kuzungumza na wanahabari.



Na Dotto Mwaibale


Mwenyekiti wa Good News for All Ministtry (Great Vition 2000), Askofu Dk.Charles Gadi anatarajiwa kuongoza mkutano mkubwa wa kuliombea Taifa utakaofanyika kuanzia Julai 19 katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametajwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.



Makonda anatarajiwa kuzindua mkutano huo wa maombi hayo ya siku 1,001 ambayo  yataendelea kufanyika siku ya Jumanne ya kila wiki.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo 

Dar es Salaam leo, Askofu Dk. Charles Gadi alisema maandalizi ya  maombi hayo yamekwisha kamilika na kuwa yanakuja kufuatia mengine ya siku elfu moja na moja ya kuliombea taifa yaliyokwisha kufanyika  mwaka 2012 na kukamilika mwaka 2015.

Alisema "Tunakumbuka tulianza maombi ya siku elfu moja mwaka 2012 ambapo yalitimiza mwaka 2015, tunashukuru Mungu kwamba yote tuliyoyaorodhesha katika mahitaji ya siku hizo 1,001 yametimizwa na mengi yako mbioni kutimizwa". 


Alisema katika siku 1,001 wanakusudia kuombea mambo 16 yakiwemo kuombea wananchi wawe na utayari wa  kulipa kodi, kuhamasisha wanachi kujiunga na mifuko ya jamii, watunze na kulinda miundombinu ya taifa, matumizi endelevu ya ardhi, kuhamasisha utalii wa ndani, wananchi kupenda kupima afya zao mara kwa mara na wawe na tabia ya kujiwekea kumbukumbu ya hesabu ya shughuli zao.



"kuhamasisha  wananchi kulinda maadili ya taifa, kuhamasisha usafi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla, kuhamasisha wanachi kupenda vitu vya hapa nchini, kuiomba serekali iwalinde na kuwawezesha wawekezaji wa ndani na kuiombea serekali iweze kununua vifaa vya kutomsha kwa ajili ya hospitali zetu " Alisema

Askofu Dk. Gadi alitumia muda huo kuwaomba wananchi na waumini wengine kutoka madhehebu na dini mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo ambao ni muhimu wa kuliombea taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani ili watu wake waweze kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi.


(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: