CUF MTWARA WANAMTAKA LIPUMBA ARUDI NDANI YA UENYEKITI,SOMA HII

Ikiwa sekeseke ndani ya chama cha wananchi CUF likianza kufukuta juu ya kurudi au kutorudi kwa aliyekuwa mwenyekiti wao Profesa IBRAHIM LIPUMBA Wanachama wa chama hicho  mkoani Mtwara wamewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wanaokutana mnamo tarehe 21 mwezi Agust mwaka huu kumkubalia kiongozi huyo arejee kwenye nafasi yake ili kukiimarisha chama hicho..Kauli hiyo inayoendelea kuleta sintofahamu juu ya sakata hilo imekuja wakati wa ufunguzi wa shina la chama cha wananchi CUF hapo jana katika mtaa wa Chipuputa manispaa ya Mtwara mikindani  ambapo walisema kuwa  tangu Prof. Lipumba atoke kwenye nafasi hiyo chama kimekuwa kikiyumba na kwamba hakuna wa kuyasimamia na kuyakemea mambo mabaya yanayotokea ndani ya chama.


Aidha Akizungumza katibu wa CUF mkoa wa Mtwara Said Kulaga alisema katika tafiti waliyoufanya kwa kipindi kifupi ndani ya mkoa wa Mtwara wamebaini kuwa wanachama wengi wanamtaka Pro. Lipumba arejee kwenye nafasi yake ili kukiimarisha chama hicho.

“Kwa niaba ya chama na utafiti nilioufanya kwa kushirikiana na viongozi wangu inaonekana watu wengi wanachama wanaunga mkono na wanaona umuhimu wa Prof Lipumba kurudi kwenye nafasi ya uongozi,kwahiyo kama mratibu wa chama mkoa natoa tamko hili kwa niaba ya mkoa wa Mtwara na viongozi wenzangu wa mkoa wa Mtwara ambao litakuja kupewa Baraka na mwenyekiti wa chama wa wilaya ya Mtwara mjini kwa niaba ya wenyeviti wa mkoa ambao wameniagiza hapa,”alisema Kulaga


Aidha alisema kuwa tamko hilo linasema CuF ni taasisi huru ya kisiasa inayoongozwa kwa mujibu wa miongozo yake kwa maana  ya katiba hivyo misingi ya katiba kama imekiukwa inapswa kufuatwa ili kumaliza changamoto zilizopo na si migogoro ili kuleta umoja.


Akizungumza mbunge wa jimbo la Mtwara mjini ,Maftah Nachuma alisema anaungana na wananchama wake waliompa ridhaa ya ubunge hivyo anaheshimu maamuzi yao kwani chama sio mtu mmoja.


“Kimsingi chama ni wanachama,chama si mtu mmoja wala si mbunge,mambo yote nayofanya nmeagizwa na chama kwenda kuyafanya nje na ndani ya bunge kwahiyo kama tamko limetolewa na wanachama ni maamuzi ya wanachama na ndio maamuzi ya wengi na wanachama ndio walioniweka mimi hivyo siwezi kwenda tofauti nao,suala la tamko  I suala la wanachama wenyewe na wefanya vikao sio kwamba wametoa  hayo matamko bila sababu ukipita huko mitaani kila mtu anamzungumzia Prof Lipumba,”alisema Nachuma


Mwanachama Fatuma Chande alisema wanamuhitaji Prof Lipumba kutokana na kuwaeleza juu ya haki zao za msingi juu ya rasilimali gesi iliyogundulika Mtwara kwani aliweza kuwaeleza haki zao na sasa wananufaika.


“Lengo letu sisi tunawatuma viongozi wa wilaya mkamrudishe Pr Lipumba kwasababu ni mpambanaji wa kusini bila kujali anatokea wapi ,tusingeweza kujua juu ya haki zetu kama za gesi kama sio Lipumba kwani alikuja hapa akatupa tasfiri ya gesi na sisi wanamtwara tukajua haki zetu na mpaka sasa tunafaidika,”alisema ChandeNaye Radhid Abdallah alisema “Sisi tumeumbwa na Mungu makundi mawili yakipigana yapatanisheni haraka,kundi lingiine likiwaonea lipigeni,sasa Pr Lipumba amejirudi na sisi tunatakiwa tukatae ugomvi,anayesema hafai huyo ni mgomvi..kukosekana kwake katika nafasi hiyo pigo kwa chama  ,”alisema Abdallah

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.