Dk. Kigwangalla akutana na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii, Watoto atoa maagizo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekutana na Wakuu wa Idara za Maenedeleo ya Jamii pamoja na ile ya Watoto katika Wizara hiyo na kupanga mikakati mbalimbali ya kiutendaji kazi.

Katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amewataka wakuu hao wa Idara kuhakikisha wanaandaa mpango kazi kabambe ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ndani ya Wizara hiyo ikiwemo kutoa maagizo maafisa Maendeleo ya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatoka maofisini na kwenda ngazi ya chini kufanya kazi hasa Vijijini.

Pia katika kukabiliana na suala la mmong’onyoko wa maadili hasa suala la vitendo vya watu kujihusisha na mapenzi ya Jinsia moja, amebainisha kuwa mikakati hiyo kwa sasa wataanzia ngazi ya chini katikakuhakikisha wanadhibiti vitendo hivyo.
“Tunataka kuhakikisha vitendo vya unyanyasi na ukatili hasa vile vinavyoanzia mashuleni tunavikomesha mara moja. Imebainika zipo baadhi ya shule watoto wanafanya vitendo visivyo fa ambavyo pia baadae vinapelekea tabia hii ya ushoga.

Hivyo miongoni mwa mikakati ni kuhakikisha tunaandaa masunduku ya maoni kwa kila shule ili kubaini vitendo hivi na vingine visivyofaa kwa Wanafunzi ambavyo vinapelekea mmong’onyoko wa maadili.” Alieleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla amekutana na wakuu hao ni katika mikakati ya kuhakikisha anasimamia ipasavyo majukumu ya Idara hizo ambazo zinaunda Wizara hiyo.
DSC_3248Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipitia madokezo mbalimbali ya Idara za Wizara hiyo muda mfupi kabla ya kukutana na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na ile Idara ya Watoto.
DSC_3261Afisa wa Idara ya Watoto, Emmanuel Batoni akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo.
DSC_3275Mkutaano huo wa Naibu Waziri na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na ile ya Watoto ukiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla DSC_3279 DSC_3288
Sehemu ya Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla
DSC_3295 DSC_3289
DSC_3281Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoaa maagizo kwa Wakuu wa Idara mbalimbali wa Wizara hiyo.(Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).
 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.