KAMPUNI ILIYOSABABISHA AJALI JANA,MABASI YAKE YAFUNGIWA NA SUMATRA


1

Mamlaka ya Usafiri Ardhini(SUMATRA) imeifungia Kampuni ya City Boy, ambayo mabasi yake mawili jana yalisababisha ajali mbaya iliyopelekea watu 30 kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.
Jana taarifa zilienea mtandaoni kuwa ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa madereva kwa kile kilichofahamika kuwa walikuwa wakifanya mchezo barabarani kwa kukimbizana huku wakipishana kuelekea kila upande, na ikapelekea kutokea kwa ajali hiyo mbaya.
Pia inasemekana kuna basi moja kati ya hayo mawili lilipigwa tochi na polisi kwa kuzidisha speed.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.