Tuesday, July 12, 2016

KITUO CHA DK. MWAKA ,FATHAGET SANITARIUM,MANDAI HERBAL CLINIC VYAFUTIWA USAJILI WAKE, WENGINE WASIMAMISHWA MIEZI SITA NA ONYO KALI

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba asili huku akiwa ameonywa na kushindwa kubadilika.
 
Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.
 
Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi habari juu hatua walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza kushoto ni Kaimu Mkurugenz Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame.
Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai
 
Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.
 
Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame akizungumza na waandishi habari juu ya utekelezaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa wanaokiuka taratibu za utoaji huduma wa tiba asili na tiba mbadala katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.
Dk. Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa ajili ya Matangazo
 
Amesema kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa kuwahoji na kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala.Imeandikwa na Chalila Kibuda.

No comments: