MAKAMU WA RAISI ATEMBELEA BANDA TWCC KUJIONEA UZURI WA BIDHAA TOKA TANZANIAMakamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassani siku ya jana aliweza kutembelea banda la chama cha wafanya biashara wanawake Tanzania TWCC aliweza kupongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na wanawake hao huku akieleza  kuvutiwa sana na bidhaa za ngozi kama viatu vya aina mbali mbali kama viatu na mikoba ya kina mama inayotengenezwa kwa ngozi inayopatikana hapa hapa na aliweza kuwapongeza wafanyabiashara wotewanaopatikana ndani ya banda la TWCC ikiwa ni mafanikio makubwa kwa chama hicho kwa mara ya kwanza kuweza kuwa na banda lake lenyewe.
Pia mama Samia ameweza kuwasifu sana TWCC kwa kuweza kuanzisha majukwaa mbalimbali ikiwa kwa sasa chama hicho kina majukwaa 11 katika mikoa 9 ikiwa ni jitihada za kuwasidia wanawake wengi zaidi na pia aliweza kuvutiwa baada ya kuona wanawake walemavu wakipewa nafasi katika chama hicho na aliweza kuwashauri watengenezaji wa bidhaa za ngozi kuwa waweze kufanya finishing vizuri kwa kuwa bidhaa zao ni nzuri na zinaweza kuuzika hata nje ya mipaka ya Tanzania.
Na kutokanana na changamoto ya kutopatikana kwa soli na mashine nzuri za kufanyia kazi hapa nchini mpaka kuweza kuagiza nchi za nje waziri wa viwanda na biashara alisema swala limeshafika kwenya wizara yake na watalifanyia kazi alisema kutokana selikali ya awamu ya nne ni ya viwanda basi itahakikisha inasaidia viwanda vidogo vidogo viweze kuwa na nguvu kubwa ili bidhaa zetu ziweze kuuzika kimataifa na kutanua wigo kwa wajasilia mali wadogo wadogo.
Catheline Chitinde ni mmoja wa wafanya biashara ndani ya banda la TWCC ambae yeye ni anahusika na bidhaa zitokanazo na ngozi anasema amefurahi sana baada ya kutembelewa na Makamu wa Raisi na yeye anaamini tatizo lao linalowasumbua la kutopatikana kwa soli litaisha.

Aidha  anasema wanachokiomba kwa serikali ni kuweza kupata maeneo ya kuuzia bidhaa zao yaani serikali ingetenga maeneo rasmi kwaajili ya kuuza bidhaa zinazotengenezwa na wajasilia mali kutoka Tanzania.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.