MAKONDA AWATOLEA UVIVU WANAOMBEZAMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , paul Makonda akizungumza ndani ya Power Breakfast ya Clouds Fm
Na Mwandishiwetu, Dar es Salaam
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameamua kuwatolea uvivu wale wote wanaosambaza
ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii.
Makonda ambaye aliamua kutenga muda na kueleza maswala kadhaa yahusuyo jiji la Dar es Salaam kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza account feki za mitandao mbalimbali kupitia jina
lake.
“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inanza na cheo changu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda sio vingine hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo” anasema Makonda.
Anasema kuwa juu ya agizo batili lililopostiwa katika mitandao ya kijami kuwa wananchi wasiokuwa na kazi  watakwenda jela sio la account yake bali yeye ameagiza wenyeviti wa serikali ya mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa
nyumba kwa ajili ya usalama wa Maeneo wanayokaa.
Anataja kuwa kutokana matatizo yaliyopo kamwe ataacha kupambana na mafisadi katika Halmashauri
zote tatu,wauza unga , wafanya biashara wa Shisha na Mashoga.
Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa wa Dar es salaam  kuwa makini na kufuata maelekezo ya wenyeviti mitaa amabayo
nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzi ngazi ya chini kabisa

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.