Tuesday, July 26, 2016

MBUNGE WA SEGEREA BONNAH KALUWA AREJESHA KIWANJA KWA WANANCHI WA KATA YA BUGURUNI

 Mbunge wa Jimbo la Segerea,  Bonnah Kaluwa (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo na wafanyakazi wa Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited iliyokodishwa kiwanja kilichopo nyuma ya Kituo cha Polisi Buguruni ambapo ametoa siku tatu waondoke kupisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni. Mapato ya kiwanja hicho kwa zaidi ya miaka 10 yalikuwa hayajulikani yalipokuwa yakienda.
 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Buguruni, Remmy Mishehe (kulia), akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu kiwanja hicho.
 Maelezo zaidi yakitolewa.
 Mmoja wa mtu aliyedaiwa ni dereva wa kampuni hiyo, akidhibitiwa baada ya kudaiwa kutoa lugha ambayo siyo nzuri mbele ya mbunge wakati wa ziara ya mbunge huyo kukagua kiwanja hicho.
 Malori ya kampuni hiyo yakiwa yameegeshwa kwenye kiwanja hicho. 
Mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo akitoa maelezo kwa Mbunge Bonnah Kaluwa (kushoto). Katikati mwenye suti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Buguruni, Barua Mwakilanga.


Na Dotto Mwaibale

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kaluwa amefanikiwa kukirejesha kiwanja kwa wananchi wa Kata ya Buguruni kilichokuwa kikitumika kuegesha magari kwa malipo bila kujulikana matumizi ya fedha hizo.

Kiwanja hicho ambacho kipo nyuma ya kituo cha Polisi Buguruni kilikuwa kimetengwa miaka mingi iliyopita kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni.

Akizungumza wakati akikagua kiwanja hicho Dar es Salaam leo asubuhi ambacho  kinatumiwa na Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited kuegesha magari yao alisema wametoa siku tatu wawe wameondoka ili waanze mara moja ujenzi wa shule hiyo ambapo jumla ya sh. milioni 40 za kuanzia ujenzi huo zimetengwa.

"Kata ya Buguruni haina shule  hata moja ya sekondari kupatikana kwa kiwanja hiki kitasaidia watoto kupata shule katika kata yao badala ya kwenda shule zingine za mbali" alisema Kaluwa.

Kaluwa aliongeza kuwa waliokuwa wakitumia kiwanja hicho waliingia mkataba na uongozi wa Kata ya Buguruni ambapo katika kipengere namba nne kilieleza kuwa ikifika wakati eneo hilo likihitajika basi mpangaji atalazimika kuondoka.

"Kwa kuwa mpangaji wa eneo hilo yupo na mkataba unajieleza wenyewe kupitia kipengere hicho tunaomba wahusika watupishe haraka iwezekanavyo tuanze ujenzi wa sekondari" alisema Kaluwa.

No comments: