.

MSANII ALBINO AJIPANGA KUTEKA SOKO LA MUZIKI,ATAMANI COLABO NA BENPOL NA LINEX,SOMA ALICHOKIZUNGUMZA LEO NDANI YA TBC FM

Msanii Abino aliyevaa T-shit nyeupe akizungumza moja kwa moja kutoka Radio TBC FM katika kipindi cha NDIO MAMBO wakati wa mahojiano yake leo 
 Na Exaud Mtei
Msanii wa muziki wa Hip Hop Tanzania anayechipukia kwa kasi GOOD MANSON maarufu kwa jina la ALBINO leo amepata nafasi ya kueleza maswala mbalimbali yanayohusu mziki wake na harakati za kuukuza  kitaifa na kimataifa Zaidi ndani ya Radio TBC FM katika kipindi cha NDIO MAMBO kinachoongozwa na watangazaji BK na JCLK.

Akizungumza katika kipindi hiko kilichorushwa na Radio TBC FM amesema kwa sasa amekwisha Rekodi nyimbo 16 kwa mfumo wa Audio katika studio mbalimbali nyingi zikiwa za mkoani arusha na moshi ambapo amesema kwa sasa ameamua kuja Jijini Dar es salaam ili kupanua mziki wake Zaidi baada ya kuona Dar es salaam ni mkoa ambao unaweza kumpa mafanikio Zaidi kimuziki.
          
Msanii huyo ambaye anatamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki yangu hela amesema kuwa katika harakati zake za kufanya muziki amekuwa akikutana na changamoto kubwa zikiwemo pia za kuweza kuwapata waandaaji wazuri wa muziki kipindi ambacho alikuwa nje ya Dar es salaam lakini kwa sasa amekuja Dar es salaam kwa ajili ya kufanya muziki hivyo akawataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani kazi nzuri zinakuja ikiwemo Video ya Nyimbo yake mpya ya Rafiki yangu hela.

Akizungumzia nyimbo hiyo yake mpya amesema kuwa Wimbo wa Rafiki yangu hela ameimba kutokana na ukweli kuwa katika maisha ya sasa kila kitu kinahitaji hela hivyo ni ukweli usiopigika kuwa katika marafiki wazuri duniani hela nayo ipo hivyo ameimba ili kuwakumbusha watanzania na vijana kutafuta hela kwa nguvu na Hari kubwa ambapo wimbo huo upo katika hatua za mwisho kufanyiwa video na kampuni ya NORTWOOD MEDIA ya mkoani chini ya THK.
          
Aidha akieleza mipango yake ya kufanya colabo na wasanii mbalimbali wa ndani ya Tanzania wanaofanya vizuri amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kufanya ngoma na msanii Benpol na linex na mipango hiyo inaendelea vizuri huku akisema anahitaji kufanya kazi na wasanii wengine Zaidi kwa kuwa mziki sasa ni biashara na sio kujifurahisha kama ilivyodhaniwa na wengi.
KUSIKILIZA WIMBO WA HELA WA MSANII ALBINO NIMEKUWEKEA CHINI HAPO

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.