SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA ELIZABETH MAYEMBA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto kutokana na kifo cha Elizabeth Mayemba - Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Majira.

Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha mwandishi huyo mwandamizi wa habari za michezo nchini kilichotokea Julai 09, 2016 na habari zake kuanza kusambaa majira ya jioni jana kabla ya kuthibitishwa na wanafamilia na uongozi wa TASWA kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.
Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Elizabeth Mayemba.
Elizabeth Mayemba, wakati wa uhai wake alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika gazeti la Majira na wakati fulani magazeti ya Kampuni ya New Habari House 2006.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Elizabeth Mayemba mahala pema peponi.

Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.