Sunday, July 10, 2016

TASWA yaomboleza kifo cha Elizaberth Mayemba


Chama


Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko 
makubwa taarifa za msiba wa mwanachama wake,Elizaberth Mayemba 
kilichotokea jana  jioni huko nyumbani kwake Tabata kwa Swai.

TASWA
imestushwa na kuhuzunishwa  sana kutokana  na kifo hiki cha  Elizaberth
ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa 
unahitajika sana.

Waandishi
wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka Elizaberth kutokana na 
ucheshi,kujituma na  uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa 
mfano kwa waandishi chipukizi.

TASWA
inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa 
habari na kuwatakia moyo wa  subira katika wakati huu wa majonzi ya 
kuondokewa na mpendwa wetu.

Mwenyezi
Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. TASWA ipo pamoja 
na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Juma Pinto
Mwemyekiti TASWA

No comments: