.

TGNP NA EASSI WATAKA WADAU MBALIMBALI KUUNGA MKONO MSWADA WA SHERIA YA USAWA NA KIJINSIA NA MAENDELEO YA JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI

Lilian Liundi Mkurugenzi wa mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP LILIAN LIUNDI akizungumza na wanahabari mapema leo 
EASSI ni asasi ya kuhamasisha mpango wa maendeleo ya wanawake katika ukanda wa afrika mashariki (EASSI) yenye miaka 20 sasa ni asasi ya kirahia ya kikanda iliyoanzishwa mwaka 1996.

EASSI ina dhamira ya kuwezesha ufuatiliaji wa utekelezaji  wa makubaliano ya jukwaa la utendaji wa Beijing (Beijing platforms for action{ BPFAS}) Ambacho ni chombo cha mkutano wa nne wa wanawake uliofanyika nchini Beijing nchini china mwaka 1995 na mkutano wa nne wa wanawake afrika uliofanyika Dakar Senegal asasi hii ambayo imesajiliwa nchini Uganda kama asasi isiyo ya kibiashra, inafanyakazi na asasi nyingine za kitaifa katika nchi nne zikiwamo Burundi, Eritrea,Ethiopia,Kenya,Rwanda,Somalia Tanzania na Uganda
Kuanzia mwaka 2008 EASS kwa  kushirikiana na mashirika yanayotetea haki za wanawake ikiwemo TGNP Mtandao na nchi tano wanachama ilikuwa ikifanya kampeni kuweza kuleta itifaki ya usawa wa kijinsia na itifaki hii iliweza kubadilishwa na kuwa mswaada binafsi na kuwasilishwa katika bunge la afrika mashariki na kuwa tayari kusikilizwa na umma katika nchi tano wanachama na lengo la mswaada huo nikukuza mahusiano ya kijamii kiuchumi na kisiasa na utamaduni kwa manufaa ya wanawake na wanaume ili kuweza kufuatwa kwa haki za binaadamu katika nchi hizo zimeridhia matamko mbalimbali kwa mfano azimio la Beijing, SEDO itifaki ya mkataba afrika kuhusu haki za binadamu  malengo endelevu ya kidunia la kwanza umasikini na la tano kuhusu usawa wa kijinsia kampeni hii ilichangizwa nchi za kusini mwa afrika SADC iliyofanywa  na wanawake kusini mwa afrika iliyowahimiza kuwepo kwa tamko au mkataba wa  kijinsia ambao baadae ilibadilika na kuwa itifaki ya kijinsia.

Mwenyekiti  wa TGNP Mtandao  Lilian Liundi amesema kuwa afrika mashariki inahitaji mswaada wa sheria kijinsia na maendeleo kwa kuwa jumuiya ya afrika mashariki imesaini mikataba mingi ya kitaifa na kikanda na pia ukiukwaji wa haki za wanawake umeendelea kushamili ndani ya jumuiya hiyo kwa mfano vitendo vya ukeketaji bado vinaendelea na kwamba kwa Tanzania ni28.4- 31.7  Kenya 27% sudan 88% Uganda 1%


Lakini pia amisema kuwa hata katika maswala ya uzazi vifo vimezidi kuongezeka kwa kiwango kikubwa sana na ametoa idadi katika wazazi laki moja wanafariki hadi 740 kwa burundi Kenya 400 Rwanda 320 Tanzania 410 Uganda 360 na pia anasema hili si la kulifumbia macho kwa kuwa ni kinyume na makubaliano ya Abuja ambayo nchi hizi ziliweza kukubali kwa kusema asilimia 15 itengwe kwaajili ya sector ya afya na akiongezea kwa kusema hii ni baadhi tu ya mifano lakini ipo mingi sana inayomkandamiza mwanamke.
Ameongezea kuwa mswaada huo itakapopitishwa itasaidia sana wanawake wengi ambao wanakandamizwa na pia itaoanisha sheria za kikanda na kimataifa  kwa afrika mashariki na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia na kuleta usawa kwa jinsia zote katika Nyanja mbalimbali kwenye maamuzi , uongozi na biashara. Pia sheria hii itawawezesha wanawake kwa wanaume kuweza kukua katika biashara na ubaguzi wa kijinsia utakuwa umetokomezwa.

Pia alisema kuwa sio tu wanasukumwa kupitisha sheria hiyo ila wanania thabiti ya kupima selikali za nchi zote wanachama kweye kutekeleza majukumu yao ya kuweka usawa wa kijinsia  kwa mara ya kwanza wame amua kuanzisha kipimo cha mlengwa wa kijinsia na pia iko kipimo litatoka na chapisho lakini pia katika hilo chapisho litakuwa na takwimu maalumu kuhusu kipimo katika nchi zote wanachama na chapisho la kwanza litatoka mwezi oktoba, lakini pia hilo chapisho halitalenga selikali pekee mfano tukisema umasikini umeshuka wataweza kutembelea wananchi nakuweza kuongea nao na kujua ni kweli kama takwimu zinavyosema au kuna udanganyifu umetendeka.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.