Monday, July 11, 2016

TGNP YAWANOA MADIWANI KUHUSU BAJETI YENYE MLENGO WA KIJINSIA NCHINI

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Liundi akifungua mafunzo ya siku tano ya madiwani mbalimbali kutoka Tanzania mafunzo ambayo yana lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya Bajeti ya Tanzania na hususani kuichambua kwa mlengo wa kijinsia ili waweze kuwasaidia wananchi wanaowaongoza
 Zaidi ya madiwani 20 kutoka katika kata mbalimbali nchini Tanzania leo wameanza kupatiwa mafunzo ya siku tano yakiwa na lengo la kuwaongezea uelewa kuhusu dhana ya bajeti kwa ,mlengo wa kijinsia na matumizi yake katika kutengeneza mipango na bajeti kupitia nafasi walizo nazo.

Mafunzo hayo maalum yamefanyika Jijini Dar es salaam ambayo yameandaliwa na mtandao wa jinsia nchini Tanzania TGNP na kuwakutanisha madiwani kutoka katika kata tofauti hapa nchini ambapo yamegfunguliwa Rasmi na Mkurugenzi wa Mtandao huo LILIAN LIUNDI.
Akifungua mafunzo hayo Liliani Liundi amesema kuwa lengo la TGNP ni kufwatilia na kunoa uelewa wa viongozi hao kuhusu maswala mazima ya bajeti ikiwa ni pamoja na kufwatilia jinsi bajeti inavyotoka na kutumika hususani bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo amesema ni bajeti ambayo inapanga Rasilimali kulingana na makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii zetu alkisisitiza kuwa  itakuwa ni bajeti ya haki kwa wananchi wote.

Amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha viongozi hao kutambua haki mbalimbali za makundi katika jamii katika Bajeti ya Tanzania na kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuongozi hususani kuitumia Bajeti hiyo katika kuwasaidia wananchi hususani  makundi yaliyopo katika jamii zao.

Baadhi ya waheshimiwa madiwani kutoka kata mbalimbali za Tanzania wakiwa wanasikiliza kwa makini mafunzo hayo ambayo yatadumu kwa siku Tano ndani ya mtandao wa TGNP Dar es salaam
Baadhi ya madiwani ambao wamezngumza na mtandao huu juu ya mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yamekuja katika wakati muafaka ambao bajeti ya Tanzania imesomwa na sasa ni kazi ya viongozi wa ngazi za chini ambao ndio wanaokwenda kuitumia bajeti hiyo hivyo wameshukuru sana waanzilishi wa mafunzo hayo kwa kuwa yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi kila siku.

No comments: