Saturday, July 9, 2016

UTEUZI WA MH MAGUFULI UMEWASAHAU WANAWAKE,TGNP WATOA YA MOYONI LEO

Liliani Liundi ambaye ni Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia nchini TGNP akizngumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam kuhusu nafasi ya wanawake katika uteuzi wa nafasi mbalimbali za kiuongozi katika serikali ya awamu ya Tano

Na Exaud Mtei
Wakati serikali ya awamu ya Tano nchini Tanzania ikiendelea na uteuzi wa nafasi mbalimbali za utumishi serikalini zikiwemo zile za wakurugenzi,wakuu wa wilaya na watumishi wengine hatimaye hoja ya kupungua kwa uteuzi wa wanawake katika nafasi hizo imeanza kuibua mijadala mbalimbali huku baadhi ya wanaharakati wakitoka hadharani na kukosoa uteuzi huo waliosema unarudisha nyuma harakati za kuleta usawa wa kijinsia.

Wiki moja iliyopota Rais wa Jumhuri ya muungano wa Tanzania DR JOHN MAGUFULI alifanya uteuzi wa nafasi za wakurugenzi wa wilaya na mikoa mbalimbali huku katika uteuzi huo ikionyesha kushuka kwa ushirikishwaji wa wanawake  jambo ambalo limeanza kuzua minongono kuwa kunahitajika usawa katika nafasi zinazotolewa na serikali kwa sasa.

Mbele ya wanahabari leo Jijini Dar es salaam mashirika takribani Kumi yakiongozwa na mtandao wa jinsia nchini TGNP yanajitokeza mbele ya wanahabari kuzungumzia swala hilo huku wakionyesha wasi wasi wao juu ya nafasi ya wanawake katika kupewa nafasi za uongozi hasa hizo za kuteuliwa na Mh Rais.
Mratibu wa kituo cha usuluhushi kutoka TAMWA ambaye ni GLADNESS MUNUO akizungumza katika mkutano huo leo
Liliani Liundi ni Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia nchini TGNP akizungumnza na wanahabari amesema kuwa ukiangalia nafasi za makatibu wakuu  utagundua kuwa kati ya 29 walioteuliwa  wanaume ni 26 ambao ni sawa na asilimia 89.7 huku wanawake wakipungua kutoka 5(asilimia 21.7) mwaka 2014 hadi 3(aslimia 10.3) kwa sasa hivyo wanawake wamepungua kwa aslimia 10,ambapo kwa upande wa manaibu makatibu wakuu idadi ya wanawake imepungua kwa kiasi kikubwa pia.
Wawakilishi wa mashirika mbalimbali watetezi wa haki za wanawake wakiwa katika mkutano huo
Aidha amesema kuwa katika nafasi za wakuu wa mikoa kwa Tanzania bara kati ya nafasi 26 nafasi 21 wamepewa wanaume ambao ni sawa na asilia 80,na wanawake 5 sawa na asilima 20 ya mikoa yote Tanzania bara ambapo kwa wakuu wa wilaya bado hali ni hiyo hiyo ambapo kwa mwaka huu wanawake ni asilima 28.89% ukilinganisha na aslimia 71.1 ya wanaume ambapo inaonyesha kuporomoka ukilinganisha na mwaka jana ambapo wanawake walikuwa 35.07%.

Amesema kuwa sasa wao kama wanaharakati wameona kama 
wataendelea kuiacha hali hiyo kuendelea itarudhisha nyuma juhudi ambazo ziloifanywa na serikali za awamu iliyopita ya kuleta usawa wa kijinsia ambapo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuanza kuwapa kipaumbele wanawake katika nafasi hizo za uongozi.
Mratibu wa kituo cha usuluhushi kutoka TAMWA ambaye ni GLADNESS MUNUO akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa hakuna serikali duniani ambayo inaweza kufikia malengo yake hasa ya kimaendeleo bila kuwapa kipaumbele wanawake kwani wao ndio wazalishaji wakubwa katika taifa lolote duniani.

Ameongeza kuwa katika uteuzi huo uliofanyika imewasikitisha sana kuona hata katika majina ambayo yametoka serikali imeshindwa hata kuwagawa na kuonyesha majina na jinsia za watu jambo ambalo linaonyesha wazi kipaumbele kwa jinsia ya wanawake sio kipaumbele kikubwa cha serikalio hii.

Mashirika hayo ambayo ni TAMWA,ULINGO,TAWLA,WAJIKI,WOFATA,TAWIA,WFT,WLAC,LISA,BINTI LEO kwa pamoja wamemtaka Rais wa Tanzania pamoja na serikalio yake kusimamia kwa vitendo mikataba ambayo imeseiniwa nan chi hususani inayohusu usawa wa kijinsia ili kupunguza pengo lililopo kuelekea usawa wa 50 kwa 50 katika nafasi za uongozi.


No comments: