VIKONGWE 394 WAUAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA TANZANIA,SOMA HII KUTOKA LHRC

Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Bi Hllen Kijo Bisimba akifafanua jambo wakati LHRC walipotoa Taarifa ya haki za binadamu nchini Tanzania kwa miezi sita iliyopita 

Na Exaud Mtei

Watu 394 wakiwemo vikongwe katika maeneo mbalimbali ya vijijini nchini Tanzania wameuawa kwa Imani za kishirikina kwa kipindi cha miezi sita kwa mwaka 2016 huku ikitajwa ni ongezeko kubwa la mauaji hayo ukilinganisha na mwaka jana ambapo ni vifo 57 tu vilivyoripotiwa nchini.

Hali hiyo imeelezwa leo katika taarifa ya haki za binadamu kwa miezi sita kuanzia January ya mwaka 2016 iliyotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania lhrc ikiwa ni utaratibu wa kituo hicho kutoa Report kuonyesha hali ya mwendendo wa haki za binadamu nchini Tanzania kwa kipindi husika.

Akizungumza wakati wa utoaji wa Taarifa hiyo mbele ya wanahabari Jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa LHRC Bi Hllen Kijo Bisimba amesema kuwa haki ya kuishi nchini Tanzania imeendelea kukiukwa kwa kasi huku mauaji ya Imani za kishirikina yakionekena kuongezeka kwa kasi.
Paul Mikongoti Kutoka LHRC akifafanua baadhi ya mambo ambayo yanapatikana katika Report Hiyo
Ameeleza kuwa pamoja na Idadi hiyo ya 394 iliyotajwa na Report hiyo bado kuna uwezekenao mkubwa kuwa matukio ni mengi Zaidi ya hayo kwa kuwa mauaji ya aina hii mengi yamekuwa hayatolewi taarifa kwenye vyombo vya dola,huku akiitaja mikoa ya Mwanza,Simiyu,Geita,Shinyanga,ikiendelea kuwa vinara wa matukio ya mauaji yanayohusisha Imani za kishirikina.

Aidha katika Report Hiyo iliyotolewa leo na LHRC imeonyesha maeneo mbalimbali ambayo bado haki za binadamu zimekuwa zikikiukwa kwa kasi kwa kipindi cha miezi sita iliyopita huku wakiitaka serikali kuhakikisha wanachukua hatua za haraka ili kudhibiti hali hiyo ambayo ikiachwa inaweza kuligharimu Taifa.

Paul Mikongoti ni Mwanasheria na mtafiti kutoka LHRC ambapo akisoma baadhi ya maeneo hayo ameeleza kuwa mwaswala kama kujichukulia sheria mikononi kwa wananchi bado ni tatizo nchini Tanzania ambapo watu 135 wameuawa kwa watu kujichukulia sheria mkononi,huku eneo lingine likiwa ni watu kufia mokononi mwa polisi ambapo Kwa mujibu wa Taarifa Rasmi ya Jeshi la polisi ni taarifa ya mtu mmoja aliyefia mikononi mwa polisi japo katika LHRC wamekiri kwa wao wanataarifa ya watu wawili Zaidi waliofia mokononi mwa polisi.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Imelda Lulu Urio Akifafafanua jambo
Maeneo mengine ni uvamizi wa vituo vya polisi,mauaji ya ukatili kwa watu wenye ualbino,ajali za barabarani,haki ya uwakilishi,haki ya wanawake na watoto,haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni pamoja na haki ya kupata habari na uhuru wa vyombo vya habari,haki za kisiasa,haki ya afya,ambapo kwa pamoja mambo hayo yameonekana kukiukwa sana katika kipindi cha miezi sita iliyopita jambo ambalo linahitaji kuangaliwa kwa makini Zaidi.

Katika eneo la haki za kisiasa Report hiyo imeeleza kuwa sakata la Jeshi la polisi kuzuia shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya kisiasa hasa ile inayofanywa na vyama vya upinzani ukiwemo ule wa CHADEMA kahama na  ambapo watu walipigwa mabomu pamoja na kongamano la ACT WAZALENDO kupigwa marufuku ni ushahidi tosha kuwa haki ya kufanya siasa nchini Tanzania imekiukwa na serikali ya awamu ya tano inahitaji kujitagfakari upya kwani kazi ya mwanasiasa ni kufanya siasa hivyo anahitaji haki hiyo.
Aidha sakata la utumbuaji majipu lililoanzishwa na serikali ya awamu ya tano likiwa na lengo la kurudisha nidhamu katika kazi nakutokomeza Rushwa limetajwa kama moja kati ya mambo yaliyokiuka haki za binadamu nchini kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukosekana kwa haki ya wale wanaotuhumiwa kupewa nafasi ya kujieleza kabla ya hatua kuchukuliwa ambapo kwa mujibu wa katiba ya Tanzania inamtambua tu kama mtuhumiwa mpaka pale mahakama itakapomkuta na hatia ndipo anaweza kupewa adhabu stahiki.About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.