Monday, July 25, 2016

ZITTO KABWE AALIKWA NA HILLARY CLINTON



Kiongozi  wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe ameondoka  Nchini kuelekea Philadelphia Nchini Marekani Kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention) utakaomthibitisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho.

Wakati Akiwa kwenye Mkutano huo Ndugu Zitto atapata Fursa ya Kufanya Mazungumzo Na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa duniani, Kufanya Kikao Cha Maandalizi Juu ya Ufunguzi wa Tawi la Wanachama wa ACT Diaspora la Nchini Marekani pamoja na Kuwa Na Mazungumzo Maalum na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad Juu ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar na Taifa Kwa Ujumla. Zitto na Maalim Seif ndio wanasiasa pekee nchini walioalikwa kwenye shughuli za chaguzi za nchini Marekani.

Taarifa zaidi zitafuata.
Abdallah Khamis
Afisa Habari, ACT Wazalendo

No comments: