Wednesday, August 3, 2016

BREAKING NEWZZ--TAARIFA MPYA KUHUSU MBUNGE TUNDU LISSU JIONI HII TENA


Kuna habari zinaenea kuwa Mbunge Tundu lissu amekamatwa na Polisi jioni Hii Baada ya kumaliza kuhutubia Mkutano Jimboni kwake.Baada ya habari hizo Mbunge huyo inasemekana huu ni ujumbe wake wa Baada ya kukamatwa
Breaking News!!!!!!! Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida. Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida nikamatwe. Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam. Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. 
It's likely nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, there's no turning back. There's no shutting up. Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail, as long as I've a voice to speak with. Sitakubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Msikubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Aluta continua! !!!!!Tundu Lissu.
BAADA YA UJUMBE HUO HII NI KAULI YA SALUM MWALIM KIONGOZI WA CHADEMA



 Wakuu salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu amekamatwa punde na Polisi baada ya mkutano Ikungi, hivi sasa wanaelekea mjini Singida ofisini kwa RC akiwa chini ya ulinzi wa Polisi na akitumia gari ya polisi baada ya kumkatalia kutumia gari yake, mliopo Singida naamini hamtomwacha mpweke Kamanda mwenzetu. 
Salum Mwalim
Naibu Katibu  Mkuu(Z)

No comments: