Saturday, August 27, 2016

MBEYA CITY FC WAMEKAMILIKA KUIANGAMIZA TOTO AFRICAN KESHO JUMAPILI

Mlinda  mlango mahiri  Owen Chaima (pichani juu) ni mmoja wa nyota  wa kikosi cha Mbeya City Fc kinachondoka leo hapa mjini Shinyanga kuelekea Mwanza  tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soska Tanzania bara dhidi ya wenyeji Toto Africans uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mapema  asubuhi hii  meneja wa kikosi hiki Godfray Katepa  amesema maandalizi yote kuelekea mchezo wa jumapili tayari yamekalika kinachosubiriwa sasa  ni dakika 90 za uwanjani siku hiyo ya mchezo ambazo anaamini zitakamilika kwa City kuibuka na ushindi na kubeba  pointi tatu  muhimu kabisa ambazo zitaisukuma  timu yake kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

“Hakika tumekamilisha  kila kitu  kuhusu mchezo huo, hii ina maana kuwa maandalizi yote  kwa vijana wetu yamekenda sawa, baada ya suluhu na Kagera Sugar tuliendelea  kubakia  Shinyanga lengo letu lilikuwa ni kupata wasaa mzuri wa kufanya mazoezi kwa utulivu, hilo lilifanikiwa  tumefanya mazoezi ya kutosha kwenye uwanja wa Kambarage, kwa sababu  tunakwenda mwanza leo tutakuwa na siku moja nyingine ya mazoezi ccm kirumba, hivyo basi  hakuna shaka kuwa tuko kamili na tayari kwa mchezo wa jumapili”.IMG-20160826-WA0002Jana jioni mazoezini Kambarage Stadium, Shinyanga.
“Timu yetu imeimarika zaidi,  hatuna shaka na kupata ushindi dhidi ya Toto, vijana wako ‘fiti’ hakukuwa na majeruhi yeyote hata baada ya mchezo uliopita pamoja na mazoezi mazito ya siku kadhaa, tunasaifiri kwenda mwanza leo kwa lengo moja tu  la kushinda  ikiwezekana kwa idadi kubwa  ya mabao”Kuhusu hali za wachezaji, Katepa  aliweka wazi kuwa nyota wote wako kwenye hali nzuri  kwa sababu hata baada ya mchezo na Kagera Sugar  hakukuwa na majeraha yeyeto kikosini hivyo uhakika wa kucheza kwa kiwango cha juu na kushinda mchezo huo ni mkubwa kutokana na uimara wa wa chezaji hivi sasa.
Kwa picha  zaidi za mazoezi kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga  ingia  hapa.

No comments: