Sunday, August 28, 2016

MBEYA CITY FC YAIFANYIA UNYAMA TOTO AFRICAN FC LIGI KUU

ct 1IKICHEZA mchezo wa pili kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu, Mbeya  City Fc imefanikiwa kuvuna pointi zote tatu muhimu baada ya kuifunga Toto Afican ya Mwanza bao 1-0 kwenye mchezo  uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba.
Haruna Shamte lifunga bao hilo mapema dakika ya 7 kwa mpira wa adhabu iliyotplewa baada ya Joseph Mahundi kuangushwa alipokuwa kijaribu kuwatoka waalinzi wa Toto African, hii ilikuwa ni baada ya mashambulizi mfululizo ambayo City iliyafanya kwenye lango la timu hiyo ya Mwanza tangu kipenga cha  kuanza mpira  kilipopulizwa.
Raphael Daud, Kenny Ally na Joseph Mahundi walicheza vizuri kwenye eneo la kiungo na kuifanya City  kung’ara vizuri uwanjani kipindi chote cha kwanza licha ya jitihada za mara kadhaa kutoka kwa wachezaji wa Toto jambo lililohitimisha  dakika 45 za kwanza  ubao ukisoma  1-0.
20160828-IMG_0050
Kipindi cha  pili,kocha  Kinnah Phiri aliwatoa  Salvatory Nkulula na Geoffrey Mlawa  aliyeumia  na nafasi zao kuchukuliwa  Ditram Nchimbi na Michael Kerenge mabadiliko ambayo  yaliongeza  nguvu ya mashambulizi kwa City lakini kupungua kwa umakini kwenye eneo la mwisho  kulihitimisha dakika 90 bao likisalia hilo 1-0.

Mara baada  mchezo huo,  Kocha  Phiri amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri, na kuwataaka kujituza na kuwa tayari kwa mchezo mwingine mwishoni mwa juma lijalo.
“Vijana wangu wameonyesha mchezo mzuri, kama ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita, kitu izuri zaidi ni kuwa leo tumepata pointi tatu, hili ni jambo jema, kwa sababu tunapata nguvu ya kupambana kwenye mchezo ujao”.

Kwa  picha zaidi za mchezo wa Toto  na City  nenda hapa…

No comments: