Sunday, August 7, 2016

RUSHWA YA NGONO NA UMASKINI CHANZO CHA MWANAMKE KUSHINDWA KUNGARA KWENYE SIASA ZA TANZANIA


Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo Spika mstaafu Mama Anna Makinda akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa  wanawake 
Wakati wanaharakati wa haki za wanawake na wadau mbalimbali wakiendelea kupambana kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi sawa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ya uongozi,rushwa ya ngono,Umaskini vimetajwa kuwa vikwazo vikubwa vinavyofanya taifa la Tanzania kushindwa kuwa na wanawake wengi katika nafasi mbalimbali za kisiasa.

Hayo yameelezwa Jijini Dar es salaam na wakawake viongozi na wanaotarajiwa kuwa viongozi katika kongamano maalum la wanawake lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP kwa kushirikiana na ACTIONAID mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake hao kupambana katika nafasi mbali mbali za uongozi nchini.


Katika Tamko lililosomwa na wakawake hao mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Spika mstaafu ya Bunge la Tanzania Mama ANNA MAKINDA wanawake hao wameeleza kuwa uwezo mdogo wa kiuchumi miongoni mwa wanawake walio wengi umekuwa kikwazo kikubwa sana katika harakati zao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za nchi na kujikuta wakishindwa kushiriki kwa ukamilifu zoezi la uchaguzi jambo ambalo linazidi kuwapa nafasi wanaume kutawala katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini.


Aidha wameeleza kuwa kwa uzoezi walioupitia katika uchaguzi kwa mwaka jana imeeonyesha kuwa  Rushwa ya ngono ilikuwepo kwa kiasi cha kuwakwamisha baadhi ya wanawake na wengine kuogopa kujitokeza katika nafasi hizo huku pia familia zikishindwa kuwaunga mkono wanawake wanaotaka kugombea kwa kile walichoita ni kuogopa aibu ya rushwa ya ngono kwa familia.

Wanawake mbalimbali wakichangia mijadala katika shughuli hiyo
Wanawake hao ambao walikutana kwa mara ya kwanza Mjini Dodoma mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu na baaadae kukutana Wiki hii kupeana mrejesho wa kile kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana wamesema kuwa wanaitaka serikali Asasi za kiraia,TAKUKURU na wadau wengine kuongeza jitihada za kukemea Rushwa ya ngono na kuongeza uhamasishaji ili iweze kuzunguziwa kwa uwazi ili kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria katika kulishughulikia Tatizo hilo.


Aidha wanawake hao wameitaka serikali kurekebisha sheria ya usajili wa vyama vya siasa ya mwaka 1992 itamke rasmi uwiano na usawa wa kijinsia katika nafasi kuu za maamuzi ndani ya vyama na pia sheria ivitake vyama vya siasa kuteua wanawake asilimia 50 kwenye kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi Taifa.

Katika warsha hiyo ambayo mgeni Rasmi alikuwa Mama Anna Makinda wengine waliohudhuria ni pamoja na Mgombea Pekee wa nafasi ya Urais mwanamke kutoka Tanzania Mama Anna Mgwira Kutoka ACT WAZALENDO,mbunge wa viti maalum kutoka CHADEMA Sophia Mwakagenda,pamoja na mkurugenzi mtendaji wa TGNP Bi LILIAN LIUNDI.

No comments: