Wednesday, August 24, 2016

SERIKALI YAJIPANGA KUKARIBISHA SEKTA BINAFSI TAZARA--TIZAMA MAONYESHO YA MIAKA 40 YA TAZARA HAPA

Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya  ujenzi Uchukuzi, na mawasiliano Bw.Aunyisa Meena,akizungumza na wadau mbalimbali ambao walifika wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo maalum ya kuadhimisha miaka 40 ya TAZARA
 
Na Vicent Macha wa HABARI24 BLOG

Serekali ya Tanzania kupitia kwa wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano imeahidi kuendelea kuisaidia mamlaka ya reli Tanzania na Zambia TAZARA katika kuboresha mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kufikia malengo na kuimarisha maeneo mbalimbali ikiwemo kuwawezesha wafanyakazi wake nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya  ujenzi Uchukuzi, na mawasiliano Bw.Aunyisa Meena, wakati akifungua Rasmi maonyesho ya siku Tatu ya mamlaka Hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanza kufanya kazi kwake ambapo amesema kuwa serikali ya Tanzania pamoja na serikali ya Zambia zimejipanga kuhakikisha kuwa zinamarisha mamlaka hiyo.
Meena amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa malengo ya kuboresha shirika hilo yanatimia serikali ya Tanzania imeanza kupitia sheria ya TAZARA ili sasa kuruhusu secta binafsi kuingia na kuwekeza ndani ya mamlaka hiyo ambapo amesema kuwa kwa kuanza mpango huo Tayari serikali ya china imeanza kusaidia katika sector hiyo huku serikali ikihitaji wadau mbalimbali watakaoweza kusaidia mamlaka hiyo kusogeza mbele maendeleo yake.
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akihutubia katika shughuli hiyo CHINA ni moja kati ya nchi ambazo zimeonyesha nia ya dhati katika kuinua TAZARA kwa sasa
Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa hali ya TAZARA inaimarika na kuwabadilisha uelewa wafanyakazi wake ikiwa ni kipindi cha ushindani hivyo jitihada kubwa za kuboresha ikiwemo kuwepo kwa mabehewa mazuri,njia nzuri,vichwa vizuri vya Treni pamoja na mbinu mbalimbali ili kufanikiwa kuwapata wateja kutoka nchi za jirani kutumia Treni za TAZARA katika kazi zake.
Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Judith Kapijimanga (kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya  ujenzi Uchukuzi, na mawasiliano Bw.Aunyisa Meena,wakati wakitembelea maonyesho ya miaka 40 ya TAZARA ambayo yanafanyika Jijini Dar es salaam
Bwana Meena ameeleza kuwa mategemeo makubwa ya serikali ni kuhakikisha kuwa katika kipindi kifupi TAZARA inaimarika huku akipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na TAZARA ikiwemo mpango wao wa sasa wa kurekebisha Engine zilizokuwa mbovu zipatazo nne na sasa kuwezeshwa kufanya kazi.
Maonyesho ya Miaka 40 ya TAZARA yalitanguliwa na shughuli mbalimbali miezi miwili iliyopia zikiwemo uchagiaji wa damu,usafi katika Hospitali mbalimbali,ambapo maonyesho ya leo yanalenga kuonyesha Shughuli  na huduma mbalimbali zitolewazo na TAZARA.
Katika uzinduzi huo leo umehudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi akiwemo Balozi wa Zambia nchini pamoja na Balozi wa China.

 







No comments: