Sunday, August 7, 2016

TANZANIA YA VIWANDA YAPEWA CHANGAMOTO,WANASAYANSI WATAKA UZALISHAJI WA WANASAYANSI WA KUTOSHA KUTOKA MASHULENI KWANZA

Mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa shirika la wanawasansi chipukizi Tanzania YST Dr Gozibert Kamugisha akizungumza na wanahabari mapema Leo Jijini Dar es salaam kuhusu maonyesho ya wanasayansi chipukizi Nchini Tanzania ambayo yatawakutanisha wanafuzi mbalimbali kwa shule za secondary kote nchini kuonyesha Bidhaa zao mbalimbali za kisayansi walizotengeneza,maonyesho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Mwalimu JK Nyerere. Jijini Dar es salaam 
 Wakati watanzania wakisubiri kwa hamu ahadi ya serikali ya awamu ya tano iliyoingia nayo madarakani ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda mpango huo umeelezwa kuwa unaweza kufeli kama serikali haitajikita katika kutengeneza wanasayansi vijana kuanzia shule za msingi na secondary ili baadae waje kuwa tegemeo katika viwanda hivyo nchini.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa shirika la wanawasansi chipukizi Tanzania YST Dr Gozibert Kamugisha wakati akizungumza na wanahabari kuhusu onesho la wanasayansi chipukizi la mwaka 2016 litakalofanyika katika ukumbi wa Julias Nyerere Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 10 hadi 11 mwezi huu wa nane tukio ambalo litawakutanisha wanafunzi mbalimbali kuonyesha kazi za ugunduzi wa kisayansi na teknologia zilizotengenezwa na wanafunzi wa shule za secondary kutoka mikoa yote Tanzania
Brian Nolan Kutoka Ubalozi wa Ireland akisisitiza jambo mbele ya wanahabari leo ambapo nchi yake pia ni moja kati ya wadau wanaofanikisha maonyesho hayo kwa kiasi kiikubwa ambapo mashindano ya BT YOUNG SCIENTISTS yatafanyika nchini kwake na washindi wa kutoka Tanzania watashiriki
Amesema kuwa mpango huo wa kuwakutanisha wanasayansi kutoka mashuleni na kuwapa nafasi ya kuonyesha kazi zao  utakuwa msaada mkubwa kipindi kijacho na hasa kipindi hiki ambacho serikali ya Tanzania inataka kuingia katika mfumo wa kuwa nchi ya viwanda huku akisema kuwa kama serikali haitaweza kuwakuza wanasayansi kutoka katika mashule na vijana mpango wa viwanda hauwezi kufanikiwa kamwe kwani wanaoendesha viwanda kote duniani kwa asilimia kuwa ni wanasayansi.
Co-Founder/Director and senior science Adverser kutoka shirika la wanasayansi chipukizi Tanzania  YST akikisiriza jambo mbele ya wanahabari
Katika maonyesho hayo yatakayofanyika Dar es salaam wanafunzi ambao watafanya vizuri kwa kuonyesha Bidhaa bora Zaidi wataibuka na zawadi mbalimbali ambapo wanafunzi wapatao 50 watashinda zawadi ya Pesa,Medali,vikombe,vifaa vya maabara na kutengeneza maktaba kwa shule itakayoshinda zawadi ya maktaba.

Kamugisha ameongeza kuwa wanafunzi wanne watashinda zawadi ya udhamini wa kushomeshwa chuo kikuu katika fani ya sayansi ili kuwawezesha kuwa wanasayansi mahiri miaka ya baadae huku akisema kuwa washindi wa Jumla wa mashindano ya mwaka huu watalipwa Gharama zote za kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya BT YOUNG SCIENTISTS huko ulaya nchini Ireland mwezi January 2017 na pia watapewa Udhamini wa kusomeshwa chuo kikuu.

No comments: