Saturday, August 13, 2016

TGNP-JITIHADA ZETU ZIMEFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KWA WANANCHI



Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akizungumza mbele ya Kamera za waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mkutano na wahariri wa habari hapa nchini. Liundi alisema dhamira kubwa ya kukutana na wakuu hao wa vyombo vya habari ni kutaka kujenga uelewa juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia pamoja na mahusiano yake katika jamii.

Afisa mipango, uchambuzi na machapisho Bw. Deogratius Temba akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika mchakato wa bajeti na utengenezaji wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia.

Mjumbe wa bodi  ya Wakurugenzi katika Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) Dk Alexander Makulilo akizungumza na  wahariri alipokuwa anafungua Mkutano huo wa siku moja wenye dhamira ya kuboresha uelewa juu ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akizungumza na Wahariri katika mkutano huo. katika mkutano huo pia Liundi alizungumzia mchakato wa ulaghabishi na jinsi ulivyoleta mabadiliko katika jamii

Mhariri wa EATV, Rwehabura Rugambwa  akichangia hoja katika mkutano huo.
Mhariri kutoka kituo cha Mlimani TV Amini Mgheni (katikati) akichangia mada katika mkutano huo . Kushoto kwake ni Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Bi. Betty  Kangonga
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari.
Wahariri wakichangia mada katika mkutano  huo.
 
Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP  umekiri kuwa jitihada za uraghabishi zinazofanywa na Mtandao huo zimefanikisha kuwasaidia wananchi kujitambua na wengine kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuatilia miradi mbalimbali inayoelekezwa katika mitaa vijiji vyao.

Akizungumza na Wahariri mbalimbali katika mkutano maalum wenye lengo la kuboresha uelewa juu ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia, Mkurugenzi wa Mtandao huo Bi. Lilian Liundi alisema katika kata ambazo walifanikiwa kufika na kuwachokoza (kufanya ulaghabishi) kuhusu rasilimali zao na jinsi wanavyoweza kufanya mabadiliko ya kimaendeleo, asilimia kubwa waliweza kubadilika na kujiletea maendeleo.

 Alisema mchakato wa ulaghabishi umeleta mabadiliko katika jamii ikiwamo kubadilisha hali yao ya kimaendeleo hususani katika sekta ya shule, maji na afya, kwani kuna baadhi za kata zilifanikiwa kubadilisha hali za shule zao kwa kupitia nguvu zao wenyewe na serikali kumalizia sehemu iliyobaki

No comments: