Wednesday, August 10, 2016

Tigo wazindua duka la kisasa mjini Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo, akikata utepe kwenye uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya Tigo Ikwiriri wilayani humo leo.Wanaoshuhudia Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles(mwenye miwani kulia),Meneja Mauzo wa Kanda ya Pwani Asnath Mboya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rufiji Rashid Salum (kushoto).
Msimamizi wa duka la Tigo la Ikwiriri Anthonia Nyalagwinda akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Juma Njwayo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya Tigo Ikwiriri wilayani Rufiji leo.




 Wakazi wa Ikwiriri mjini na vitongoji vya jirani sasa wanaweza kufurahia zaidi huduma za Tigo, kutokana na uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la Tigo lililofunguliwa leo katikati ya mji huo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa Tigo wa kanda ya Pwani , Goodluck Charles alisema, ufunguzi wa duka unaenda sambamba na mkakati wa kampuni wa kupanua na kuleta huduma zake karibu na wananchi nchini kote.
“Hili ni duka sahihi kwa wateja kwa sababu linaleta bidhaa na huduma zote za Tigo chini ya paa moja na kwa ukaribu zaidi. Pia liko katikati ya mji ambapo linarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake wanaotoka  vitongoji vya mji wa Ikwiriri, “alisema.
Duka hili jipya lililofunguliwa ni miongoni mwa maduka mengine yaliyofunguliwa nchini, ambapo linajumuisha eneo ambalo
wateja watakaokuwa wanakuja kwa mara ya kwanza watafurahia kujifunza jinsi ya kutumia bidhaa na huduma za Tigo kama vile matumizi ya simu za Smartphones, modemu za intaneti na huduma nyingine za kimtandao kama vile Muziki wa Tigo na Facebook ya bure inayotolewa na kampuni.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kanda, duka hili lililoko mtaa wa sokoni linatarajiwamkuhudumia zaidi ya wateja 300 kwa siku, “idadi ambayo itapunguza usumbufu wa kusafiri umbali mrefu ambao wateja wetu walikuwa wakiupata hapo awali katika kutafuta huduma za Tigo kwenye maduka kama hili jijini Dar es Salaam”.
Akiongoza uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Abdallah Njwayo alisema kwa kuleta huduma za Tigo karibu na wananchi, “duka hili jipya litakuwa kichocheo katika kujenga fursa mpya za kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa eneo”.
Huduma za Mawasiliano kama zile zinazotolewa na Tigo kama kupiga simu, ujumbe mfupi, kuunganisha intaneti, kufanya miamala ya fedha kwa njia ya simu za mkononi na nyinginezo zimekuwa zikichochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, alisema Njwayo huku akiwaasa wakazi wa mkoa wa Pwani kutembelea duka hilo ili kujipatia huduma mbalimbali zilizosogezwa
karibu yao.

No comments: