Tigo yatangaza punguzo bei ya tiketi, vifurushi vya bure Fiesta 2016

 Mratibu wa fiesta, Shafii Dauda  akiongea na waandishi jinsi ya  kulipia tiketi ya fiesta kupitia Tigo Pesa na katikati ni Meneja chapa wa Tigo, William Mpinga , Kulia ni na Mtaalam wa mitandao ya jamii wa Tigo, Samira Baamar.

Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo uliofanyika mapema  leo jijini Dar es salaam.
Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania ambaye anapenda kushirki katika tamasha la Fiesta 2016  mdhamini mkuu wa tukio hilo la aina yake Tigo Tanzania leo imetangaza  punguzo la asilimia kumi  kwa tiketi  itakayonunuliwa  kwa Tigo Pesa kwa msimu huu wa Fiesta.
Tofauti na matukio  yaliyotangulia, washiriki wote kutyoka mtandao wowote kwa tamasha la mwaka huu watakuwa na chaguo la kuzipata tiketi zao kupitia Tigo Pesa  bila tozo za ziada.
Tiketi hizo zitawawezesha washiriki kulifikia kwa urahisi tamasha hilo ambalo litaanza rasmi Agosti 20, 2016 jijini Mwanza. Bei kamili za tiketi zitatangazwa hivi karibuni.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika Tip Top Manzese, Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga alisema, “Njia ya  kulipia tiketi  kupitia Tigo Pesa  lengo lake kubwa ni kuwapatia Watanzania  njia rahisi na ya kawaida  ya kupata tiketi zaoambayo ni ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania.”
Mpinga alibainisha kwamba  huduma hiyo mpya imepanda chati  kufuatia hivi karibuni kampuni hiyo ya simu  kuanzisha kampeni ya NitigoPesa ambapo mtu yeyote kutoka  mitandao mingine mikubwa nchini Tanzania  anaweza kutuma na kupokea pesa  kutoka kwa mteja wa TigoPesa.
Meneja chapa huyo  aliongeza kwamba ikiwa kama kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo inawahakikishia  kuwa  kwa kununua  tiketi kupitia Tigo Pesa, wateja kutoka Tigo na mitandao mingine wataweza  kuzifurahia huduma za Tigo Pesa bila tozo zozote za ziada.
Mpinga alieleza ili  kununua tiketi  kwa Tigo Pesa wateja kutoka mtandao wowote  anatakiwa kupiga namba ya mfumo wa kifedha kwa njia ya simu (mfano: *150*01# kwa  Tigo),  chagua “Tuma Pesa” halafu chagua, “Mitandao mingine”, ikifuatiwa na, Tigo Pesa na hatua ya mwisho  ingiza namba: 0678 888 888.  Mbali na  punguzo la asilimia kumi, wateja wa Tigo ambao watanunua tiketi za Fiesta  kwa Tigo Pesa pia watapata  kifurushi cha zawadi cha thamani ya shilingi 20,000 ambacho kinajumuisha dakika 400, SMS 400 na MB 400 zitakazotumika ndani ya siku saba.
Aliendelea kusema, “Kwa wateja wa mitandao mingine  tiketi itakayonunuliwa kwa Tigo Pesa kutoka mitandao mingine  watapata kadi ya 4G ikiwa na dakika 60 SMS 60 na MB 60 papo hapo  pamoja na dakika nyingine 400, SMS 400 na MB 400 zitakazotumika ndani ya siku saba zikianza kutumika  ndani ya saa 24”.
Huku akiwakaribisha Watanzania wote kushiriki katika Tamasha hilio la Fiesta, Mpinga aliwashauri  washiriki kununua  tiketi zao  mapema ili kuepuka usumbufu  unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho.
 Tamasha la Tigo Fiesta 2016 linafanyika kwa ushirikiano kati ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania  ambaye ni mdhamini mkuu.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.