BREAKING NEWZZ--TETESI ZA LIPUMBA KUHUSISHWA KUJIUNGA ACT WAZALENDO ,SOMA KINACHOENDELEA HAPA

Habari ambazo zimeanza kuenea mitandaoni kuanzia asubuhi ya jumatatu ya leo ni kuhusu Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Pro Ibrahim Lipumba akihusishwa kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO.
 
Habari hizo zimechagizwa zaidi na Baadhi ya maafisa wa ACT WAZALENDO kutumia mitandao ya kijamii kumnadi kwa kasi Mwenyekiti huyo wa zamani wa CUF aliyejiondoa mwenyewe.
Moja ya maafisa wa kitengo cha mawasiliano wa ACT WAZALENDO ameonekana akitumia mitandao kutuma baadhi ya post za kumuonyesha LIPUMBA akiwa na ZITTO huku akiandika maneno ambayo yamekuwa yakiibua midadala kwa watanzania.

Habari nyingine ni kuhusu Kikao cha ndani acha ACT ambacho kimeanza leo kinachofanyika kwa usiri mkubwa huku Kiongozi Mkuu wa ACT WAZALENDO akiwaahidi wanahabari kuwa Taarifa rasmi juu ya kikao hicho itatolewa Muda ukifika.

ZITTO KABWE amekanusha hakuna mwanachama mpya anayejiunga na chama hicho na wala hakuna ajenda kama hiyo inayojadiliwa ndani ya kikao hicho.
2/2 hatuna mjadala kuhusu wanachama wapya.Mkumbuke tu hao wanaoeneza tuna wanachama wapya ndio hao hao walisema hivyo hivyo 2015. Ikawaje?

Labda kuna kikao kingine kujadili Hilo. Sio hiki nilichomo Mimi sasa hivi 
Kikao cha Kamati kuu ya Chama kinaendelea. Narudia - hakuna ajenda ya kumpokea Kiongozi yeyote wa chama kingine
Wataalam wa siasa wanasema ni muda wa kusubiri na kuona Je nini Kitajiri na kujua Ukweli na uongo wa jambo hili

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.