TUNDU LISSU ATUPA JIWE JINGINE GIZANI--TIZAMA KAULI ZAKE NGUMU KUHUSU WATU WALIOKAMATWA NA KUTESHWA

Mh. Tundu Lissu azungumzia kukiukwa kwa sheria.
Asema zaidi ya watu kumi(10) wanashikiliwa polisi kwa zaidi ya wiki mbili kinyume na sheria inayowataka polisi kumshikilia mtuhumiwa kwa Masaa ya yasiyozidi 24 bila kupandishwa mahakamani.


Haki inapatikana Mahakamani na si kitu cha Polisi. Amewaombwa waandishi wa habari kupaza sauti ili Dunia na Ulimwengu ujue juu ya ukiukwaji wa sheria wa waziwazi ambao serikali hii chini ya mtukufu/mtakatifu wa nchi wamekuwa wakiambiwa kuna uvunjwaji wa sheria bila kuchukua hatua.

Ni watanzania wenzetu ambao wametimiza haki yao ya kutoa maoni.
OCD, RPC na RPC hawana mamlaka bali kesi hizi zinazotokana na kusema vibaya mtukufu wa nchi zimeamliwa kusimamiwa na DCI na si mwingine.

Watu hawa inasemekana wameteswa sana, wamepigwa sana, wakiwa Dar es Salaam (Mikocheni) kipo kikosi kazi kwa ajili ya kutesa watu. Wanavuliwa nguo na kupigwa. Wamesema haya yote mbele ya OCS baada ya Mimi(Tundu Lissu) kuwatembelea kuhoji.
Sheria (katiba 13 (6)e za nchi zinasema ni marufuku MTU kuteswa, kuadhibiwa kinyama ama kudhalilishwa. 

Jeshi la nchi wamekuwa wana endelea kutumiwa na serikali kuwanyamazisha wananchi wanaotoa maoni ama kuikosoa serikali. Jiulize karne hii inafanya haya, ni aibu sana.

Hatua tutakayochukua, kama itafika siku ya Jumanne bado hawajaachiliwa kwa dhamana ya polisi ama kuwapeleka mahakani tutakwenda mahakama juu ambayo inauwezo wa kuamuru mahakama yoyote kuwaitwa wakuu wa vituo waende mahakamani wakajieleze kwa nini wana endelea kuwashilia watanzania zaidi ya muda ambao sheria imepanga pia wajibu kwa nini wanawatesa wakati mamlaka hiyo kikatiba inazuiliwa?

Katiba ya nchi kwa majibu ya sheria ya magazeti. Kwa majibu huo kuipinga serikali inapokosea si kosa la Jinai wala si uchochezi.
Hawana hatia tokea Uhuru pamoja na marais mbalimbali na katiba ya nchi hii ipo wazi.

Watanzania tunahaja ya kupaza sauti na kuungana kuyapinga haya kwa vitendo, Mungu anaona ataendelea kujibu kwa vitendo.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.