ACT WAZALENDO KUFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA KIDEMOCRASIA KESHO UKUMBI WA MAKUMBUSHO


 

CHAMA Cha ACT wazalendo kesho Oktoba 8/2016 kitafanya mkutano wake mkuu wa kidemokrasia  katika ukumbi wa makumbusho uliopo maeneo ya Posta jijini Dar esSalaam.

Mkutano huu ni hitaji la kidemokrasia ya Chama cha ACT Wazalendo ibara ya 29(7) kupitia katiba yake toleo la  2015
Katika mkutano huo mada mbali mbali zitawasilishwa na viongozi wa Chama hicho,ambapo Zitto Kabwe atawasilisha mada juu ya hali ya nchi kwa mtazamo wa Chama cha ACT wazalendo


Mwenyekiti wa Chama Mama Anna Mghwira atawasilisha mada juu ya uzoefu wa chama cha ACT Wazalendo kwenye uchaguzi mkuu wa 2015,hasa akitumia uzoefu wake alioupata katika uchaguzi huo baada ya kuzunguka maeneo mengi ya nchi kipindi cha uchaguzi

Mshauri wa Chama Profesa Kitila mkumbo atawasilisha mada juu ACT Wazalendo kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 pamoja na uchaguzi mkuu wa 2020
Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji Hussein Ruhava atawasilisha mada juu ya siasa ni maendeleo na namna chama cha ACT wazalendo inavyobadilisha maisha ya watu wa kigoma ujiji hasa ikichukuliwa kuwa manispaa ya kigoma ndiyo manispaa pekee nchini inayoongozwa na ACT Wazalendo.

Mbali na watoa mada kutoka ndani ya Chama pia mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania(JUKATA) Deus Kibamba na Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Omar Said Shaaban watatoa mada juu ya uzoefu wa mchakato wa katiba Tanzania na wapi nchi imekwama  na namna ya kujikwamua
Wageni Mashuhuri kutoka nje ya nchi ni Vitalis Kamerhe Spika wa zamani wa Bunge la Kongo na kiongozi wa chama cha UNC, akishirikiana na Ababu Namwamba ambaye ni kiongozi wa chama cha Labour cha nchini Kenya  kila mmoja atatoa uzoefu wa mchakato wa katiba katika nchi zao na Afrika kwa ujumla

Pia vyama vyote vya siasa vilivyopata usajili wa kudumu na ule wa muda vimealikwa kuhudhuria mkutano huo
Mkutano huu wa Kidemokrasia utaanza saa tatu kamili asubuhi

Imetolewa na Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT wazalendo
leo Oktoba 7/2016

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.