Sunday, October 9, 2016

Binslum Tyres yaipiga 'Jeki' Kandanda Day 2016

Kombe la Kandanda Day ambalo hushindaniwa kila mwaka likiwa juu ya tairi

Kampuni ya uuzaji matairi nchini ya Bin Slum Tyres Ltd,imeendeleza utamaduni wake wa kulidhamini tamasha la ‘Kandanda Day’,ambalo litafanyika Oktoba 15,mwaka huu katika uwanja wa Jakaya M Kikwete  Park,Kidogo Chekundu.

Mratibu wa tamasha hilo,Fatma Dahir,amesema kwamba wanaishukuru kampuni hiyo inayoongoza kwa uuzaji matairi nchini kwa msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya tamasha hilo linalobebwa na kauli mbiu Dawati na Mpira.

“Kwanza kabisa tunapenda kuchukua fursa hii,kuishukuru sana kampuni ya Bin Slum,kwa kutuamini na kuwa pamoja zaidi ya miaka miwili katika kuhakikisha tamasha hili linaendelea kuboreka mwaka hadi mwaka,”alisema na kuongeza
Picha ya pamoja wakati wa kukabidhiana Jezi zitakazotumika katika Tamasha la Kandanda Day 2016. Kutoka kushoto: Cet Njovu, Salim Said Al Jabry, Eric Zomboko (Dizo Moja) na Fatma Dahir
“Kwa mwaka huu,kauli yetu mbiu ni Dawati na Mpira, ambayo lengo lake kuu ni kuhakikisha sisi kama wanamichezo tunaunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha shule zetu zina madawati ya kutosha,hivyo tunaamini kwa ushirikiano wa wanamichezo wanaounda kundi la Kandanda kwenye ukurasa wa facebook na wadau wengine,tunaweza kuchangia kitu kwa ajili ya elimu yetu.”

Fatma alisema,kwamba wanaamini udhamini wa fedha walioupata kutoka Bin Slum,utakua chachu ya ulifanikisha tamasha la mwaka huu,kuwa bora zaidi na kuweka historia kwa wanamichezo watakaoshiriki na shule itakayopata msaada wa madawati.
Cet Njovu (Wa pili kutoka kushoto) akipokea Jezi kwa Niaba ya Team Ismail kutoka kwa muwakilishi wa Kampuni ya BIN SLUM TYRES, Bwana Salim Said Al Jabry. Kulia ni Bi Fatma, Mratibu wa Kandanda Day
Kwa upande wa mwakilishi wa kampuni ya Binslum Tyres Ltd, Bwana Salim Said Al Jabry, alisema kwamba wameamua kuendeleza utamaduni wao wa kuchangia tamasha la kandanda pamoja na kuuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati nchini.

“Binslum Tyres tunafuraha kubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya udhamini,ikumbukwe huu ni mwaka wa tatu  kwa kampuni yetu kudhamini  tamasha hili,ambalo kwetu ni faraja kuona wadau wanakutana pamoja na kushiriki pia kuisaidia jamii kupitia mchezo wa kandanda,”alisema Al Jabry na kuongeza:
“Kwa hiyo mwaka huu mbali na kutoa jezi kwa timu mbili mwenyeji ya Team Dizo Moja na Team Ismail,lakini pia tumetoa kiasi cha fedha kipatacho milioni moja kwa ajili ya kuchangia mchango wetu wa madawati na shughuri zingine za uendeshaji.”

Mwaka huu tamasha hilo linatarajia kushirikisha timu mbalimbali za makampuni ambazo zitacheza katika mfumo wa ligi,kab­­­la ya mshindi kupatikana katika mchezo wa fainali.

No comments: