.

Breaking Newz---Msajili na Lipumba wafikishwa mahakamani,Cuf watinga mahakama kuu

 Wakati sakata la nani ni nani ndani ya cha,ma cha nwananchi Cuf Likiendelea kuchukua sura Mpya kila kukicha hatimaye leo sakata hilo limetua meza ya mahakama kuu ta Tanzania likiwa na sura ya kupinga kile ambacho kinadaiwa kufanywa na Aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kabla ya Kujiuzulu kwake Profesa Ibrahim Lipumba.

Katika makahakama kuu Jijini Dar es salaam mtandao huu umeshughudia wakili wa chama hicho JUMA NASSOR  akiwa katika mahakama hiyo kuiwakilisha Bodi ya wadhamini wa chama hicho ambao ndio wanafungua kesi hiyo ya kuitaka mahakama hiyo kuweka ziuo maalum kwa msajili wa Vyama vyavya siasa kuacha kufanya kazi nje ya mipaka yake ambapo wanalalamikia msajili kuingilia maswala ya chama hicho kinyume Taratibu zake.

Akizungumza na wanahabari nje ya Mahakama kuu Juma Nassor amesema kuwa mbali na kuweka zuio kwa msajili wa vyama vya siasa pia kesi hiyo imelenga waliokuwa wanachama 12 wa chama cha wananchi Cuf wakiongozwa na Profesa Lipumba.

Hadi mtandao huu unaleta Report Hii bado kesi hiyo ilikuwa haijafunguliwa kutokana na kuendelea kukamilishwa kwa Taratibu mbalimbali za kimahakama.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.