Dk.Kigwangalla aombewa dua na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla jioni hii ya leo Oktoba 13.2016 amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla,   Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.
dsc_1216Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akiwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia) wakati wa kuombewa dua maalum usiku huu.
dsc_1211Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (kulia) akimuombea Dua maalum Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla (kushoto aliyefumba macho)

dsc_1207Dua zikiendelea
Dk.KigwangallaMbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akibusu mkono wa Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
dsc_1202Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuaga Dk.Kigwangalla baada ya dua
dsc_1243
dsc_1199Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akiombewa dua katika tukio hilo
dsc_1218Watu kutoka Mataifa  mbalimbali  Duania ikiwemo jamii ya Bohora ambao pia wapo hapa nchini nao wamepata bahati ya kuombewa dua maalum na Shehe huyo Mkuu
dsc_1228Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akitoka katika tukio hilo la kuombewa dua
dsc_1225Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akitoka katika tukio hilo la kuombewa dua 
dsc_1230dsc_1242Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba  akisalimiana na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla  wakati wa tukio hilo
dsc_1237Picha ya pamoja 
dsc_1167Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi  Kigwangalla akipata picha pamoja baadhi ya vijana ambao walipata kufunga ndoa na wake zao ndoa ambazo zaidi ya 50 zimefungwa huku Shehe Mkuu huyo wa Mabohora Duniani pia alipata kuzibariki.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.