Scorpion, mwenye fulana nyekundu, akiwa mahakamani leo chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Leo katika mahakama ya wilaya ya Ilala, mkazi wa buguruni kwa mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama Scorpion amepandishwa kizimbani na kusomewa tena shtaka la unyang’anyi  wa kutumia silaha .
Kesi ya Scorpion, ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa mabibo Hostel, inasikilizwa na hakimu Adolf Sachore.
Leo kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo mtuhumiwa amerudishwa rumande