Kubwa Dar es salaam leo--Mamia waandamana kukumbuka hili muhimu

 Watanzania wametakiwa kuhakikisha kuwa wanaishi katika njia za kumpendeza mwenyezi mungu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maswala ya kuboresha hali ya jamii yanayopewa kipaumbele,kukata tamaa,kuamrisha mema,pamoja na kukemea maovu kama mauaji ya walemavu wa ngozi ,matendo ya kijambazi,ubakaji,ikiwa ni njia ya kumuenzi Imam Hussein aliyekuwa mbele katika kukemea mambo hayo.
Wito huo umetoleaa leo Jijini Dar es salaam na Kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala wakati akiongoza mamia ya waislam katika maaandamano ya Amani Jijini Dar es salaam ya kumkumbuka Aliyekuwa Mjukuu wa Mtume Muhammad ambaye aliuawa Kinyama na kifo chake kubakia kuwa Historia katika maisha ya waislam Duniani.

Sheikh Jalala amesema kuwa Imam Hussein aliwafunza watu namna ya kupinga ukandamizaji,dhuluma,katika jamii pamoja na kutetea haki za wanyonge hivyo ni wakati wa wananchi wa Tanzania kuanza kufwata maneno yake na kuhakikisha kuwa wanaenzi yale mema aliyoyaacha katika jamii.

Kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akizngumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo ya amani ya kukumbuka Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad Imam Hussein.Maandamano ambayo yamefanyika Jijini Dar es salaam
Ameongeza kuwa matembezi ambayo wameyafanya leo yalikuwa na lengo la kuwakumbusha watanzania kuwa na upendo umoja na mshikamano kwa kila jambo katika jamii na pia kuwapa ujumbe waislam na wasio waislam juuu ya mambo aliyoyafanya Mjukuu huyo wa Mtume,matembezi ambayo yemeanzia maeneo ya ilala Boma na kuishia Msikiti wa Shia Kigogo.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.