Friday, October 14, 2016

MBUNGE WA SINGIDA MJINI AMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA


Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya kipimo cha ugonjwa wa Malaria

Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara

 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake

 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima
 Shukrani na Pongezi
 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kijijini Mtamaa kwa ajili ya mkutano na kukabidhi kifaa maalumu kwa ajili ya kupimia Malaria

 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mtamaa
 Baadhi ya wananchi wakifurahia kifaa cha kupimia Malaria
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano

Na Mathias Canal, Singida

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.

Tatizo hilo sugu limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili nchini Kenya.

Mhe Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.

Sima alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.

Sima Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.

Alisema kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.

Sima ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.

Kuhusu kadhia ya uduni wa upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Mtamaa A Mbunge huyo amesema kuwa hadi kufikia mwezi aprili mwakani maji yatakuwa yameanza kutoka ili kumaliza kadhia hiyo kwani mradi mkubwa wa maji utakuwa umemalizika.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo kwa kufanya mkutano wa tatu katika eneo hilo tangu aingie madarakani huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha shughuli za maendeleo.

Chima amesema kuwa Mbunge huyo ni muwakilishi mzuri wa shughuli za wananchi wake na ameonyesha uwezo mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutetea hoja na kusimamia misingi ya uwajibikaji.

Naye mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai amesema kuwa kifaa hicho maalumu kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni madhubuti na imara hivyo kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali wa karibu kilomita 20 kwenda kupima ugonjwa huo.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, April 1922 katika Kijiji cha Butiama Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

Maadhimisho ya Mwalimu Nyerere hufanyika kila mwaka ambapo watanzania popote ulimwenguni huadhimisha kwa sala na matembezi mbalimbali kama ishara ya heshima kwa muasisi wa Taifa lao.

No comments: