Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afunga rasmi kongamano la 30 la Wanasayansi Watafiti

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefunga rasmi Kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) lililokuwa la siku tatu Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla amewaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa Serikali inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa nchini hivyo  uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na watu wake hasa katika Nyanja za kiuchumi, Afya, Mazingira na mambo mengine  ya kimaendeleo.

Aidha, amebainisha kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu ambapo ameahidi amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana nao katika kulipitia ufumbuzi.

Dk.Kigwangalla amewahakikishia Wanasayansi hao  kuwa, masuala yote ya kuimalisha huduma za Maabara katika ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa akilifanya kila mahala anapokwenda kwenye ziara zake juu ya upatikanaji wa huduma  Maabara bora kwenye sehemu za Afya.

“Nimependa maombi yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za msingi. Suala hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo vya Afya na Hospitali zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa sababu nina aamini kutoa huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti za Maabara ni kuchezea afya za watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na huduma bora za Maabra zetu na suala hili tutakaa mimi na Mh. Waziri kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema Dk.Kigwangalla.

Aidha,  Dk. Kigwangalla aliwatunukia vyeti maalum wanasayansi  Vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.

Kongamano  hilo  la siku tatu, Oktoba 4-6, awali lilizinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan ambaye pia aliwahakikishia Wanasayansi Watafiti hao  kuwa Serikali inatambua mchango wao na wataendelea na juhudi za kuwalinda kwani ni nguzo muhimu ya kufikia malengo ya millennia ya ukuaji wa kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela amesema kufikia tamati ya kongamano hilo ni ishara tosha maandalizi yake yalikuwa mazuri na washiriki wote walioshiriki wamejifunza mengi  huku wakiwa ni mfano wa kuigwa kwa elimu walioipata hapo.

Nchi  mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika ambapo  washiriki zaidi ya 300 wameshiriki  huku mada zaidi ya 220 zikiwasilisishwa na kujadiliwa kwa pamoja na wataalam hao.

Nchi ambazo zinashiriki kongamano hilo kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani, Bangladesh, Thailand na wenyeji Tanzania.

dsc_0653Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wanasayansi watafiti (Hawapo pichani) walioshiriki kongamano la 30 Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kongamano hilo la siku tatu.
dsc_0670Baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano hilo
dsc_0563Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) wkaiwa meza kuu.  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela 
dsc_0570Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela 
dsc_0581Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela akielezea machache kabla ya kumwalika mgeni rasmi  kufunga mkutano huo
dsc_0600Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpa shada la maua mmoja wa Staff member kwa namna walivyoweza kuandaa kongamano hilo
dsc_0606Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi shada la maua mmoja wa wafanyakazi wa NIMR kwa namna walivyoweza kufanikisha shughuli hiyo. dsc_0614Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
dsc_0620Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
dsc_0623NNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo mmoja wa Wanasayansi waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hino hilo
dsc_0626Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
dsc_0632Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo mmoja wa Wanasayansi waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
dsc_0637Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
dsc_0644dsc_0647Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akifunga rasmi kongamano hilo. dsc_0689Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari mara baada ya kufunga rasmi kongamano hilo la 30.
dsc_0699Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiagagana na wenyeji wake mara baada ya kumaliza kwa kongamano hilo.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.