Monday, October 3, 2016

NCHIMBI ‘AIMALIZA’ MWADUI FC – Mbeya City Council FC

ditBAO LA dakika ya 27 kipindi cha kwanza lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa kati Ditram Nchimbi, lilitosha kuhitimisha dakika 90 za mchezo namba  50  wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliozikutanisha  Mbeya City fc dhidi ya wageni Mwadui Fc kwenye uwanja wa Sokoine  jijini Mbeya matokeo yaliyomuacha  kocha  wa Mwadui Fc  akitangaza  kujiuzuru kufundisha pia  kujihusisha na mchezo wa soka hapa nchini.




Kwenye mchezo huo uliokuwa  na kasi ya aina yake, timu zote zilianza dakika 45 za kwanza kwa nguvu kubwa iliyoacha mashambilizi ya kila mara pande zote mbili lakini uimara wa walinda milango, Owen Chaima na Shaban Kado ulifanya washambuliaji wa timu zote kushindwa kufunga mabao ya mapema.
Dakika ya 27, mpira ulioanzia  upande wa kulia kwa John Kabanda aliyefanikiwa kuupitisha vizuri katikati ya uwanja kwa nahodha Kenny Ally, ulifanikiwa kufika kwenye miguu ya Ditram Nchimbi ambaye  akiwa nje kidogo ya eneo la 18 la Mwadui Fc alifumua shuti kali lililomshinda kipa Kado na kutinga wavuni moja kwa moja,kuandika bao la kwanza kwa City lililodumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.
dit-2Kipindi cha pili, kocha wa City Kinnah Phiri alifanya mabadiliko kwa kumtoa, Joseph Mahundi na nafasi yake kuchukuliwa na Hamidu Mohamed pia  alimtoa Omary Ramadhani na kuingia Salvatory Nkulula huku Rajab Zahir aliyepata majeraha  akimpisha Ramadhani Chombo, mabadilliko  yaliisaidia timu yake  kuimarisha safu ya kiungo na hatimaye kufanikiwa kukamilisha dakika 90 matokeo yakibaki kama yalivyokuwa.
Mara baada ya mchezo kocha msaidizi Mohamed Kijuso, alisema  wachezaji wake wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo jambo lililochangia kupatikana kwa ushindi huu.
“Mchezo ulikuwa mzuri, vijana wamecheza kwa kufuata maelekezo ya Mwalimu, hili limetusaidia kuibuka na ushindi,hatukuwa vizuri kipindi cha pili lakini safu yetu ya ulinzi ilisimama imara kufuta makosa  yote, huu ni wakatri mwingine wa kuijiandaa na mchezo ujao  kwa sababu  tayari tuna nguvu  na ari kubwa kufuatia  ushindi wa leo “alisema.
Katika hatua nyingine  kocha wa Mwadui Fc , Jamhuri Kihwelo alitangaza  kujiuzuru kuifundisha  timu hiyo huku akiapa kutokujihusisha tena naa mchezo wa soka nchini kwa kile alichookita kuchoshwa na upindishaji wa sheria 17 za soka  aliyodai unafanywa kwa makusudi na waaamuzi wa soka licha ya kukiri kutokuwa na tatizo lolote na bao alifungwa kwenye mchezo wa jana.
Kocha Julio alisema kuwa ameaamua kuachana na soka la nchi hii kwa sababu haoni dalili za kusonga mbele kutokana na matatizo ya watu wacheche huku akijisifu kwa kupata mafanikio makubwa kwenye kazi yake hiyo aliyoifanya pia kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo Qatar, Yemen na nchi kadhaa  za  Falme za kirabu.

No comments: