Friday, October 21, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

maab3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
maab1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza kushoto.

No comments: