SHEIKH MUHAMMAD ABDI WA SHIA ITHNASHERIYA AONGOZA WAISLAM KUCHAGIA DAMU KWA AJILI YA WENYE UHITAJI

Naibu kiongozi Mkuu wa waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akiwaongoza waumini wa Dini hiyo kuchangia damu kwa watanzania wanaohitaji damu ikiwa ni zoezi ambalo limefanyika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mjukuu wa mtume Muhammad (s.a.w.w) Imam Hussen (a,s) ambaye naye alijitolea Damu yake kwa ajili ya kutetea haki na Ubinadamu na kupinga kila aina ya unyanyasaji na dhuluma anayofanyiwa mwanadamu.Zoezi hili limefanyika katika msikiti wa Kigogo Post mara baada ya swala ya Ijumaa.

Naibu kiongozi Mkuu wa waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi  akipata maelekezo mbalimbali kutoka kwa Afisa uhamasishaji wa mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya mashariki Bwana Lucas Michael wakati akijiandaa kuchangia damu katika zoezi ambalo limefanyika Mara baada ya swala ya ijumaa katika msikiti wa Kigogo Post Jijini Dar es salaam

Lucas Michael ni afisa uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu salama Kanda ya mashariki akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo ambapo amewashukuru sana waumini hao kwa kuona umuhimu wa kuchangia damu kwa wingi kwani Bado Tanzania kuna uhitaji mkubwa sana wa Damu  huku akiwataka watanzania mbalimbali,Taasisi binafsi na za umma kuiga mfano huo na kutenga muda wa kuchangia damu kwa ajili ya watanzania wenzetu wenye uhitaji mbalimbali.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.