Friday, October 14, 2016

SMART KUTOA Wifi YA BURE TAMASHA LA KANDANDA DAY LEO UWANJA WA KIDONGO CHEKUNDU

Mratibu wa Tamasha la Kandanda Day (Katikati), Fatma Dahir, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mwisho ya kandanda day ambayo itafanyika katika viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park, Oktoba 15 Mwaka Huu. 

KAMPUNI ya simu za mikononi ya Smart,inatarajia kutoa huduma ya bure ya mtandao  wa  Wifi  katika tamasha  la Kandanda  Day,litakalofanyika leo,katika Uwanja wa Jakaya M Kikwete Youth Park,Kidogo Chekundu.

Mratibu wa tamasha hilo,Fatma Dahir,alisema kwamba maandalizi kuelekea tamasha hilo yamekamilika na wanaishukuru kampuni ya  Smart kwa kuwawekea wanakandanda huduma ya kuperuzi mtandao wa intaneti bure wakiwa uwanjani.

“Tunapenda kuwatangazia wanakandanda wote kuwa maandalizi yamekamilika kila kitu,halikadhalika tunapenda pia kuishukuru kampuni ya Smart,kwa kuamua kusherehesha tamasha letu kwa kuwawekea huduma ya ‘free wifi’ kwa watakaohudhuria,”alisema Fatma na kuongeza:
“Halikadhalika,napenda pia kusisitiza timu  shiriki ambazo ni Akiba Commercial bank,Taswa Fc,Coca Cola,Smart,Dar City Fc,Team Dizo Moja na Team Ismail,zijitahidi kuwahi mapema,ili tuweze kufanikisha lengo letu katika muda tuliopanga.”

Tamasha hilo ambalo lengo lake kuu ni kuchangia madawati kwa shule teule ya  msingi ya  Msumi,linapambwa na kampuni ya matairi ya Bin Slum Tyres Ltd,Smart,Coca Cola,Galacha na kituo cha House of Blue Hope.   

No comments: