Tuesday, October 25, 2016

UJUMBE KUTOKA UN KWENDA KWA VIJANA WOTE

Vijana nchini wametakiwa kuwajibika katika kukidhi maitaji yao ya kimaisha ili kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha yao na jamiii kwa ujumla.
Akizungumza katika mkutanano wa maadhimisho ya miaka 71 ya UN ,Ndugu alvaro rodriguez amesema ongezeko la vijana na mahitaji yao ni moja ya changamoto hapa nchini wanawajibika katika kujiendeleza nakuendeleza taifa ilikupata maendeleo chanya katika maisha yao, ilikufanikisha hayo vijana wanahitajika kuhakikisha kuwa na ufahamu na taaluma ili kuwezesha mabadiliko ya uchumi nchini.

Pia vijana wasisahau wao ndio chachu ya amani ha maendeleo ivyo wao kama umoja wa mataifa watashirikiana na vijana kuhakikisha wanakuwa wadau wakanuni na taratibu zilizosababisha kuwepo kwa umoja wa mataifa ili kuakikisha hakuna kijana anayeachwa nyuma katika maendeleo.



Aidha wamechukua hatua kuhakikisha vijana wanajua na kutambua malengo ya dunia uku ikiwa hivi sasa vijana zaidi ya elfu kumi wanatambua malengo hayo ivyo umoja wa matiafa unatengemea kuelimisha vijana wapatao elfu 50 ifikapo mwaka 2017 pia mashirika ya umoja wa mataifa yametengeneza program maalumu zinazohakikisha vijana hawaachwi nyuma katika kuendeleza fikra na utendaji utakao leta mabadilikiko kiuchumi ifikapo mwaka 2030.

No comments: