Ikiwa ni siku kadhaa
tangu mwenyekiti wa chama cha wananchi cuf anayetambulika na msajili wa Vyama
vya siasa nchini Profesa Ibrahumu Lioumba kufanya maamuzi ya kufukuza baadhi ya
wakiurugenzi wa chama hicho hatimaye Menyekiti wa kamati ya uaongozi wa chama
hicho Julius Mtatiro ameibuka na kufichua siri ya kufanyika kwa maamuzi hayo
huku akimtuhumu Msajili wa vyama vya siasa kuendeleza kile anachokiita
kukihujumu chama hicho.
Akizngumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam Mtatiro ameeleza kuwa kuna kikao ambacho
kiiliwakutanisha msajili wa vyama vya siasa Jaji Fransis ,Mutungi pamoja na
Lipumba ambaye wamempachika jina la Bwana yule,kikao ambacho kilempa maelekezo
kadhaa Lioumba kwa ajili ya kufanikisha kile wanachodai ni hujuma.
Amesema kuwa kabla ya
kikao hicho Aliyekuwa Mbunge wa chama hicho ambaye alisimamishwa na Chama hicho
Magdalena Sakaya ambaye yupo upande wa Lipumba alifika ofisini kwa msajili
kupata maelekezo kuhusu ni jinsi gani Ruzuku ya chama hicho itaweza kuwafikia
wao na sio chama jambo ambalo lilimfanya msajili kuitisha kikao na Lipumba kwa
ajili ya kumpoa maelekezo kadhaa.
Akieleza maazimio ya kikao
hicho ambacho wamedai kukifwatilia wamesema kuwa msajili alimuelekeza Mh
Lipumba kuhakikisha anavunja uongozi wa chama hicho kwa kuanza na kufuta
wakurugenzi hao na kuteua wengine wakurugenzi feki na mara baada ya kukamilisha
zoezi hilo aitishe Baraza kuu feki lifanye maamuzi feki ya kuvunja Bodi ya
wadhamini ambayo imeudwa na baraza kuu la Taifa la chama na mara baada ya hapo
hili baraza lake ambalo wanaliita Feki lifanye kazi ya kuwadhibitisha hao
wakurugenzi feki walioteuliwa na Mh Lipumba.
Mh Mtatiro ameendelea
kuusema kuwa Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa imemhakikishia Profesa Lipumba
kuwa kama akipita katika swala hilo la kuunda baraza kuu feki kitakachofwatia
ni kazi ya msajili kutambua kila maamuzi yatakayokuwa yanatolewa na Baraza hilo
la Mh Lipumba.
Kwa mujibu wa Mtatiro
amewaeleza wanahabari kuwa Baraza kuu la chama hicho lipo moja lenye wajumbe 53
ambao ndio waliokutana Zanzibar na
kufanya maamuzi ya kumtimia uanachama mwanachama mwenzao Lipumba na wote
waliohukuwa kwenye kikao hicho walisaini wajumbe 43 walioshiriki huku wengine
kumi wakitoa udhuru maalum.
Amesema kuwa kwa mujibu
wa katiba ya chama hicho Profesa Lipumba hata akitumia huo uenyekiti wake
aliopewa hana uwezo wa kuitisha baraza kuu la Cuf kwa kuwa baraza kuu la chama
lenye wajumbe 53 ndilo lililofanya maamuzi ya kumtimua uanachama wake ndani ya
chama.
No comments:
Post a Comment