Sunday, October 16, 2016

WAHITIMU ST. EMMANUEL CHAMAZI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM WAASWA KUZINGATIA ELIMU

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya ST. Emmanuel High School, Ernest Masaka, akizungumza katika mahafali ya saba ya Kidato cha Nne yaliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata  ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahali hayo, Katibu wa Diwani huyo na Lucy Peter, mke wa Mkurugenzi wa shule hiyo.
 Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, akizungumza katika 
mahafali hayo. Kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Ally Mkamba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata na Katibu wa Diwani.
 Taswira ya meza kuu kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu wa kidato cha nne wakionesha vyeti vyao.
 Mahafali yakiendelea.
 Ndugu na Jamaa yake mhitimu Winfrida Komba wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Walimu wa shule hiyo wakishiriki kwenye mahafali hayo.
 Wazazi na walezi wa wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu hao wakionesha jinsi ya kujifunza somo la Sayansi.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakipata burudani kupitia madirishani.
 Burudani zikiendelea kutolewa na wahitimu hao.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Katibu wa Diwani (kulia), akitoa vyeti kwa niaba ya diwani huyo.
 Mwanafunzi akikabidhiwa cheti na Katibu wa Diwani wa Kata ya Chamazi.
Katibu wa Diwani wa Kata ya Chamazi, akimkabidhi cheti mhitimu, Winfrida Komba katika mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba.

Na Dotto Mwaibale

WAHITIMU wa Kidato cha Nne mwaka 2016 katika Shule ya St. Emmanuel iliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam wametakiwa kuzingatia elimu ili kutimiza ndoto za maisha yao badala ya kujihusisha na vitendo viovu na utoro.

Mwito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata wakati akiwahutubia wanafunzi hao kwenye  mahafali ya saba ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

"Zingatieni masomo yenu ili mtimize ndoto za maisha yenu ya baadae, wazazi wenu wanawalipia ada ni vizuri mkawaonesha mafanikio yenu katika elimu na sio tabia mbaya," alisema Karata ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Alisema kwa maisha ya leo bila ya kuwa na elimu kuna changamoto kubwa ya maisha hivyo aliwaasa wahitimu hao kufanya bidii ya kusoma hata watapokuwa kidato cha tano na sita na elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Ernest Masaka aliwaomba wazazi kushirikiana na uongozi wa shule katika kuwalea wanafunzi hao wawapo nyumbani na shuleni.

"Ushirikiano baina ya wazazi, wanafunzi na walimu ni muhimu sana katika kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kupata elimu bora hivyo nawaombeni tuendelee kushirikiana," alisema Masaka.

Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba alisema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe.

Alisema licha ya shule hiyo kuwa na mafanikio, changamoto ndogo ndogo zinakuwepo lakini wanajitahidi kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja na wazazi.


No comments: