WANANCHI WA MTAA WA MCHIKICHINI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM LEO WAANDAMANA KUPINGA UJENZI WA MRADI WA UMEME ULIOPITA JUU YA NYUMBA ZAO PASIPO KULIPWA FIDIA ZAO.


 Eneo ambalo kuna kiunganishi cha kutoa umeme mkubwa na kupitisha kwenye nguzo kubwa na kupeleka ubungo kwa ajili ya kusambazia wateja umeme huo.


 Diwani wa Kata ya Mchikichini Joseph Ngowa akizungumza na wananchi wa eneo la Mchikichini kuhusu mgogoro huo uliojitokeza.(PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)


 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mchikichini,Amini Mbwana,akizungumza na wananchi wa mtaa huo kuhusu mradi wa ujenzi wa umeme unaoendelea kujengwa katika mtaa wao bila ya wao kulipwa stahiki zao. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)


 Askari polisi wakiwa kwenye sehemu ya tukio kulinda amani iwepo katika eneo la Mchikichini. 


 Mkazi wa Mtaa huo,Mariamu Iddy akizungumza na uongozi wa mtaa huo mbele ya Diwani wa Kata ya Mchikichini Joseph Ngowa (hayupo pichani) kwa niaba ya wananchi wenzake dhumuni la wao kukusanyika eneo hilo kwa ajili ya kuishinikiza Tanesco kuwalipa stahiki zao kabla ya kumaliza mradi huo.(PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)

 Wakazi wa Mtaa wa Mchikichini wakiwa wamekusanyika mbele ya kituo cha Umeme cha Karume Ilala kushinikiza mradi wa umeme wa kilovolti 132 usimamishwe kwa kuwa hawakalipwa stahiki zao na umeme huo umepita juu ya nyumba zao. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mradi wa umeme katika eneo la Mchikichini wilayani Ilala.

NA ELISA SHUNDA,DAR
WANANCHI wa kata ya Mchikichini iliyopo Wilaya ya Ilala wamefanya maandamano hadi kwenye kituo cha umeme cha Tanesco zilizopo eneo la Karume wilayani hapo kwa kushinikiza shirika hilo la umeme kusitisha ujenzi wa nguzo za kupitishia umeme mkubwa unaoendelea kwenye eneo hilo la mchikichini ambapo nyanya zake zimepitia juu ya nyumba za watu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa eneo hilo na Jambo Leo wamesema kuwa wanashangaa ujenzi wa mradi wa kupitisha umeme mkubwa ukiwa unaendelea pasipo kuambiwa endapo ujenzi huo ukikamilika wao stahiki zao watazipata wapi hivyo wanaiomba serikali sikivu ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli kuingilia kati suala hili ambalo bado halijapata muafaka wake.

Mkazi wa eneo hilo Aisha Mohamed alisema kuwa wamekuja katika ofisi hizo za tanesco zilizopo Karume Ilala kwa ajili ya kutaka kupata ufumbuzi wa tatizo walilonalo la ujenzi wa mradi wa umeme wenye moto mkali pasipo kupewa maelekezo ya malipo yao jinsi itakavyokuwa kwa kuwa mradi huo unakaribia kukamilika na nyaya za umeme zimepita juu ya nyumba zao hivyo ni hatari kwa maisha yao.

“Sisi wananchi ambao mradi huu wa umeme umepita kwenye nyumba  zetu na kama unavyoona nyaya zinamaliziwa kuwekwa pasipo kufahamu tutalipwaje stahiki zetu ili tuhame halafu kingine kinachotusikitisha viongozi wa tanesco wanaokuja katika eneo hili la mradi unapojengwa wanawaambia mafundi wao msiwe na hofu endeleeni na kazi hawa wananchi tayari tumeshawalipa fedha zao hatuelewi wanakusanyika eneo hili kwa nini wakati tumeshamaliza nao pia tulienda ofisi za wizara ya Nishati na Madini tukaonana na Dk.Paranju naye akasema sisi tumeshalipwa tayari akatuonesha mafaili yaliyokuwa yanaonesha majina yetu tuliyolipwa wote” Alisema Aisha

Pia Mkazi mwingine wa eneo hilo aliyekumbwa na kadhia hiyo Mwalimu wa Shule ya msingi ya Mchikichini,Eliver Nanyango alisema kuwa kabla ya mafundi hawajaanza kupandisha minara alienda kuwauliza mnataka kufanya nini wakamuambia wanataka kuweka nguzo za umeme mkubwa akawaambia mbona sisi hatujashirikishwa wakamjibu kuwa wameambiwa tayari wameshalipwa fedha zao hivyo wanapaswa wananchi hao waondoke kwenye eneo hilo.

“Wakati naendelea na majibizano na mafundi wa umeme waliokuja kwenye eneo la tukio kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kupandisha vyuma vya nguzo za kupitishia umeme mkubwa akatokea mzungu mmoja ambaye ni fundi kwenye mradi huo akawaambia wale mafundi there are some lady this side tell them to move out tell them please yule injinia akaenda kumuambia yule mwanamke toka nje ni hatari wewe kukaa ndani wakati vyuma vinapandishwa juu watu siku hiyo hatukuingia ndani kwa kuogopa kujeruhiwa na vyuma vile hadi saa kumi jioni walipoondoka watoto walikaa na njaa” Alisema Nanyango

Akizungumza kuhusiana na tukio hilo la wananchi wa mchikichini kukusanyika kwenye eneo la kituo cha umeme kushinikiza kusimamishwa kwa mradi huo mwenyekiti wa mtaa huo,Amini Mbwana,alisema kuwa wakati zoezi hilo likianza wahusika wakuu walikuwa ni wananchi na maafisa wa tanesco kilichotokea ni kwamba ujue eneo hili kuna kata mbili ambazo ni kata ya mchikichini na Jangwani hivyo kilichokwamisha zoezi hili lisiendelee ni kata ya jangwani ilikuwa bado haijakamilisha majina ya wananchi wake ambao mradi wa umeme umepita juu ya nyumba zao hivyo niwatoe hofu wananchi zoezi la uhakiki linaendelea vizuri kila mwananchi atalipwa hela yake kulingana na nyumba aliyonayo kwa thamani yake.

Akiongeza kutokana na sintofahamu hiyo ya wananchi wa mtaa wa mchikichini kukusanyika kushinikiza kusimamishwa kwa ujenzi wa mradi wa umeme mkubwa Diwani wa Kata ya Mchikichini,Joseph Ngowa ni kweli kuna mradi wa umeme wa kilovolti 132 unaanzia shule ya msingi mchikichini kuelekea sekondari ya Jangwani na mradi huo unapita kwenye makazi ya watu hivyo tanesco walipata nyumba 36 ambazo mradi huo umepitia hivyo tanesco waliziweka nyumba hizo kwenye sehemu tatu ambazo zipo ndani ya msongo mkubwa wa kilowati 132 unaokwenda ubungo kwenda mchikichini.

HABARI HII IMEANDALIWA NA ELISA SHUNDA KUPITIAWWW.ELISASHUNDA.BLOGSPOT.COM MAWASILIANO 0719976633 AUelisashunda@gmail.com

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.