ANNA MGWIRA ANAGOMBEA UENYEKITI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA--HII NI KAULI YA CHAMA CHAKE


TUNAMUUNGA MKONO ANA MGHWIRA KATIKA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazalendo ( ACT Wazalendo ) amepitishwa kugombea Uenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania. Baraza la Vyama vya Siasa Ni Chombo kilichoundwa Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Kwa Lengo la kuweka jukwaa la Vyama hivyo kujadiliana masuala yenye maslahi Kwa Taifa na uimarishaji wa Mfumo wa Vyama vingi nchini. Baraza hili linawakilisha Vyama vyote vyenye usajili wa kudumu.

Anna Elisha Mghwira alikuwa Mgombea Urais pekee mwanamke kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na alishika nafasi ya tatu nyuma ya Mgombea wa chama cha mapinduzi ( CCM ) na Muungano wa Vyama vya UKAWA. Katika uchaguzi huo Ni Mgombea pekee aliyeonyesha uwezo mkubwa wa kufafanua ilani ya chama chake yenye sera madhubuti Za kuleta Maendeleo ya wananchi kupitia itikadi sahihi ya Ujamaa wa KiDemokrasia.

Anna Elisha Mghwira Ni mwanasheria kitaaluma akiwa na shahada ya uzamili ya Sheria Za Haki Za binaadam. Ni mhadhiri wa chuo kikuu na mwana harakati wa jinsia. Atatumia uzoefu wake kuimarisha Baraza la Vyama vya Siasa Kama Chombo cha kuhakikisha Sheria ya Vyama vya Siasa inafanya Kazi yake ipasavyo na Kama jukwaa la kusuluhisha misuguano miongoni mwa Vyama vya Siasa nchini. Kwa hakika atapandisha hadhi ya Baraza la Vyama vya Siasa Kwa kuhakikisha Kila chama kinakuwa na sauti inayostahili kwenye Mfumo wa uendeshaji wa Nchi.

Chama cha ACT Wazalendo kinamwunga mkono Kwa dhati Mwenyekiti wa Taifa katika kinyanganyiro hiki na kumtakia Kila la kheri. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 19 Disemba 2016.
Ado Shaibu
Katibu wa Kamati yaItidikadi, Mawasiliano na Uenezi 
ACT Wazalendo

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.