Tuesday, December 20, 2016

BENKI YA KCB TANZANIA YACHANGIA KIASI CHA SHILINGI 48, 064,958

Afisa Biashara wa benki ya KCB Tawi la TFA, Arusha, Amedeus Tumaini akitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Shilingi Milioni 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation.

Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 48,064,958 kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Mch. Godsave Ole Megiroo (kushoto), ikiwa ni msaada wa fedha zilizotolewa na benki hiyo kusaidia uboreshaji wa mazingira ya shule ya Mairowa Integrity katika ujenzi wa vyoo na eneo la kufulia.  Wapili kushoto ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Mairowa Integrity Bi. Elizabeth Mollel na mwalimu wa shule hiyo BiNancy Mseli (watatu kushoto).

Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamni ya shilingi 48,064,958 kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Mch. Godsave Ole Megiroo (kushoto). Pamoja nao kwenye picha ni wafanyakazi wa benki ya KCB Tawi la TFA, Arusha.

Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Shilingi Milioni 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation. Katikati ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Mairowa Integrity Bi. Elizabeth Mollel na mwalimu wa shule hiyo Bi Nancy Mseli.  



   Mchango huo kuwezesha ujenzi wa vyoo na eneo la kufulia katika shule ya Mairowa Integrity.

Benki ya KCB Tanzania imekabidhi rasmi mchango wa shilingi 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation ikiwa ni mwitiko kwa ombi la Taasisi hiyo  kwa ajili ya ujenzi wa vyoo 16 vya kuflashi na eneo la kufulia katika shule ya Mairowa Integrity iliyo chini ya uongozi wa taasisi hiyo. Benki ya KCB ilikua imeshawasilisha mchango huo tokea mwezi wa tatu mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB, Hogla Laizer alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Bi. Laizer alisema na kubainisha kwamba tangu ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

Akitolea mfano wa michango iliyotolewa na benki hiyo katika kuboresha huduma za elimu nchini, Bi. Lazier alisema: “Kupitia miradi hiyo benki ya KCB Tanzania imeshatumia shilingi milioni miatatu kusaidia shule zaidi ya 20 kwa kuzipatia madawati pamoja na vifaa vingine vya kuboresha huduma na mazingira ya shule.”


Alimaliza kwa kusema benki ya KCB ina kawaida ya kutembelea shule zote ambazo imepeleka misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada husika. Hivyo aliieleza taasisi hiyo kuwa matunzo na matumizi mazuri ya mchango uliotolewa, ndo itaifanya benki ya KCB iongeze msaada katika shule ya Mairowa Integrity iliyo chini ya uongozi wa Ereto East Africa Foundation.

No comments: