Monday, December 5, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 2 Desemba 2016.


DSE Kushinda Tuzo za NBAA (NBAA Awards 2016)

Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limejipatia ushindi wa Tuzo ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa kufikia kiwango cha juu cha uandaaji wa vitabu vyake vya mahesabu (Best Presented Financial Statements Award for the year 2015 for the Financial Services Capital Markets Category). Tuzo hizi zinaandiliwa kila mwaka na NBAA katika juhudi za kuboresha utawala bora na uandaaji sahihi wa mahesabu kwenye taasisi za binafsi na za serikali. 
DSE imejipatia ushindi katika kitengo cha Huduma za Kifedha katika Masoko ya Mitaji. 

Mauzo ya Soko (Hati Fungani)
Mwezi wa Novemba umefunga kwa rekodi ya kuwa mwezi wa Pili katika mwaka wa hesabu wa 2016 kwa kuwa na mauzo ya juu katika soko la hati fungani baada ya mwezi Julai. Mwezi wa Novemba umefunga na idadi ya mauzo ya Tzs Bilioni 44.4, Zaidi ya asilimia 47%. Mwezi Julai uliongoza kwa idadi ya Mauzo ya Tzs Bilioni 45.7


Mauzo ya Soko (Hisa)
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa katika wiki iliyopita imeongezeka Zaidi ya mara mbili (x2) hadi Laki Mbili (262,598) kutoka Laki Moja (101,809) wiki iliyopita. Kwa upande mwingine mauzo yalishuka hadi kufikia Tzs. 200 Milioni.

Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     CRDB kwa asilimia 84.44%
2.     DSE kwa asilimia 8.66%
3.     SWIS kwa asilimia 3.04%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa makampuni kwa ujumla ulishuka hadi kufikia Trilioni 20 na kwa makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 8.1 wiki hadi wiki.

Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 5,031 wiki hadi wiki.

Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 2,770 wiki hadi wiki.

Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

No comments: