MCHEZAJI WA MBAO FC AFARIKI UWANJANI BAADA YA KUGONGANA NA BEKI WA MWADUI FC LIGI YA VIJANA TANZANIA.

mbao-ggggggggggggggggggggggggggggMshambuliaji wa timu ya vijana wenye chini ya miaka 20 wa timu ya  Mbao FC, Khalfan Ismail amefariki baada ya kugongana na kuanguka uwanjani.
Mechi hiyo ilikuwa inachezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambako michuano ya vijana chini ya miaka 20 inaendelea.
Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC wakati wakiwania mpira na kuanguka na juhudi za kuokoa maisha yake zilionekana kukakwama na Wakati mauti yanamkuta Ismail, alikuwa ameifungia goli timu yake ya Mbao FC dhidi ya  Mwadui.
Pamoja na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kagera, taarifa baadaye zilizopatikana zilieleza, Ismail alifariki palepale uwanjani.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.