Thursday, December 8, 2016

SBL yakabidhi mradi wa maji wa 83m/- Makanya wilayani Same



Mkuu wa wilaya ya same Bi Rosemary Semanyole akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi wa serengeti breweries Limited .kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasialiano wa SBLJohn Wanyancha  mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha makanya..Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika kijiji cha Makanya wilaya ya same mapema jana.
Mkuu wa wilaya ya same Bi Rosemary Senyamule akimtwisha moja ya wanakijiji ndoo ya maji kuashiria kuanza kwa mradi wa maji ulidhaminiwa na Serengeti Breweries Limited katika kijiji cha Makanya.. na kulia ni Meneja miradi wa SBL Hawa Ladha,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika kijiji cha Makanya wilaya ya same mapema jana.

Baadhi ya wanakijiji wa same wakipata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza
Baadhi ya wanakijiji wa same wakipata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza

Same, Desemba 8th, 2016- Kampuni ya Bia Serengeti leo imezindua  mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 83  katika eneo la Makanya wilayani Same  ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.

Ukiwa na uwezo kwa  kuhudumia watu 10,629, mradi huo unajumuisha  kisima  pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji  ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila saa moja.

Akizungumza katika  hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha  alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni mionmgoni mwa  mikakati kama hiyo  ambayo kampuni hiyo ya bia  imeiendesha  katika mikoa ya  Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha  zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

 Wanyancha alisema kwamba mradi wa Makanya  sio tu kwamba  utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia  utaongeza tija katika kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake  ambao  hawatahitaji kutumia saa nyingi  kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule  wakiwa huru.”

 “SBL  ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo lake  kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Wanyancha akielezea vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo wa mahusiano  aliendelea kusema SBL ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita  imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na maisha ya jumuia zao.

Wanyancha  alisema kutokana na juhuzi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 1000 na hili limechangia  katika kukua kwa kampuni  na kukuza  kipato cha wakulima.”

Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia katika kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia  malipo ya kodi ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususani  katika kutoa  huduma  ya maji  safi na salama ndani ya nchi.”


Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule aliipongeza SBL  kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika mno, akisema kwamba kampuni hiyo ya bia  imekuwa mstari wa mbele katika kukuza  miradi ya maendeleo nchini  ambayo inawezesha kuwepo kwa jamii  inayozalisha na  iliyo na afya.

No comments: